Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) kwa kusisitiza nafasi ya kimkakati ya tukio la Ghadir katika kulinda asili na usafi wa dini, alisema:
"Kama lisingekuwepo tukio la Ghadir, basi dini ingeweza kupotoshwa tangu miaka ya mwanzo."
Katibu Mkuu wa Jumuia ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) katika kikao na Imam wa Msikiti Mkuu wa Mji wa Niamey alisisitiza umuhimu wa kuimarisha Umoja wa Kiislamu na kuunga mkono nafasi ya Wanazuoni wa Dini katika jamii.