Kwa mujibu wa Ripoti Kutoka Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-: Ayatollah Reza Ramadhani, Katibu Mkuu wa Jumuia ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (a.s), ambaye amefanya ziara nchini Niger kwa mwaliko wa viongozi wa kidini wa nchi hiyo, alikutana na Sheikh Jibril Kranta, Rais wa Jumuiya za Kiislamu nchini Niger na Imam wa Msikiti Mkuu wa mji wa Niamey, na kuendesha mazungumzo ya pande mbili.
Katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na wanazuoni mbalimbali kutoka Niger, Sheikh Jibril Kranta alimshukuru Ayatollah Ramezani kwa kuhudhuria mji wa Niamey, mji mkuu wa Niger. Katibu Mkuu wa Jumuia ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (a.s) alisisitiza umuhimu wa umoja wa Kiislamu katika mazungumzo yake na Imam wa Msikiti Mkuu wa Niamey. Ayatollah Ramadhani pia alimshukuru Sheikh Jibril Kranta kwa kujali masuala ya familia nchini Niger, kushughulikia changamoto za familia, na pia kwa kuwa nguzo ya msaada na hifadhi kwa wananchi wa Niger.
Mwisho wa kikao hicho, Katibu Mkuu alimpa Sheikh Jibril Kranta pete ya baraka kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi wa Iran kama ishara ya heshima na mshikamano.
Ni vema kutajwa kuwa, ziara ya Katibu Mkuu wa Jumuia ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (a.s) nchini Niger inajumuisha mikutano na wanazuoni, wataalamu, wasomi na vijana wa nchi hiyo.
Your Comment