wanazuoni
-
Safari ya Kuleta Umoja ya Ayatollah Ramezani nchini Niger; Mazungumzo na Maulamaa Wakuu wa Dini wa Mji wa Niamey | Zawadi ya Pete ya Baraka Yatolewa
Katibu Mkuu wa Jumuia ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) katika kikao na Imam wa Msikiti Mkuu wa Mji wa Niamey alisisitiza umuhimu wa kuimarisha Umoja wa Kiislamu na kuunga mkono nafasi ya Wanazuoni wa Dini katika jamii.
-
Ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kwa mkutano wa kumbukumbu ya miaka mia moja (100) ya kuanzishwa upya kwa Chuo cha Dini cha Qom:
Ayatollah Khamenei: Jukumu la (Hawza) Chuo cha Kidini ni Kuchora Mipaka Mikuu na Midogo ya Ustaarabu mpya wa Kiislamu
"Kazi kuu na ya msingi ya Hawza ni (البَلاغُ المُبین) kufikisha ujumbe wa dini kwa uwazi na ufasaha (ubalighi wa wazi - Kwa maana: Kufikisha ujumbe kwa uwazi na uthabiti na kwa namna ambayo haiachi shaka yoyote -). Miongoni mwa vielelezo vyake muhimu kabisa ni kuchora na kueleza kwa uwazi mistari (mipaka) mikuu na ya kando ( au midogo) ya ustaarabu mpya wa Kiislamu, pamoja na kuifafanua, kuieneza, na kuikuza katika jamii kama sehemu ya utamaduni."
-
Ripoti ya Kina ya Mkutano wa 3 wa Kimataifa wa Wanahabari wa AhlulBayt(as)kwa Ushiriki wa Wanahabari kutoka zaidi ya nchi 20 za Afrika +Picha na Video
Sambamba na Siku Kumi za Karama (The Ten Days of Karama), Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa 'Waandishi wa Habari wa Ahlul-Bayt (a.s)' umefanyika leo Alhamisi asubuhi, tarehe 1 Mei, 2025), katika ukumbi wa mikutano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) Mjini Qom, kwa Ushiriki wa Wanaharakati wa Habari na Wasomi kutoka Iran na Bara la Afrika.
-
Utamaduni wa Kisasa wa Mauaji ya Kimbari ya Mawazo na Imani
"Mashambulizi ya Kitamaduni hayako tena katika kiwango cha tahadhari au nadharia; leo hii yamejikita katika kona za fikra za kijana wa Kiiran na kwa utulivu, lakini kwa mfululizo, na yanashambulia imani, utambulisho na mtindo wa maisha ya Kiislamu."
-
Je, Mazungumzo Kati ya Mwanamume na Mwanamke Wasiokuwa Mahramu Yamekatazwa kwa namna yoyote ile katika Uislamu?
“Kauli yenye nguvu zaidi ni hii kwamba kusikia (kusikiliza) sauti ya Mwanamke asiyekuwa Mahram, maadamu si kwa ajili ya tamaa, starehe au maslahi, ni jambo linaloruhusiwa (linajuzu). Vivyo hivyo kwa Mwanamke, ikiwa hakuna hofu ya fitina, anaweza kusikika na Wanaume wasio mahram kwake".
-
Marasimu ya kuhuisha Mikesha ya Siku za Lailatul-Qadr itafanyika katika Haram ya Hadhrat Zainab (s.a)
Marasimu (Sherehe) ya kuhuisha Usiku wa Lailatul- Qadr itafanyika kwa muda wa nyusiku tatu katika Madhabahu (Haram) Tukufu ya Hazrat Zainab (s.a).