Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (ss) -ABNA-: Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlul-Bayt Uturuki katika taarifa yake imelaani vikali mipango yoyote ya Marekani ya kuingilia au kumdhuru Kiongozi Mkuu, na imesisitiza kuwa jambo hilo ni mstari mwekundu kwao.
Katika tamko hilo wamesema:
Leo ubinadamu, hasa ulimwengu wa Kiislamu, unapitia moja ya nyakati nyeti zaidi katika historia. Mipaka kati ya haki na batili imekuwa wazi zaidi kuliko wakati wowote, si Mashariki ya Kati tu bali duniani kote, na sasa kuna kambi mbili zilizosimama ana kwa ana.
Kwa kila mwenye akili na dhamiri ni wazi kuwa bendera ya dhulma na uistikbari imo mikononi mwa Shetani Mkubwa, yaani Marekani, pamoja na zao lake haramu, utawala ghasibu wa Kizayuni. Upande wa pili kuna kambi tukufu ya mapambano ya kupinga dhulma chini ya uongozi wa hekima wa Imam Khamenei, kama kinara wa kambi ya haki, kwa ajili ya kusimamisha uadilifu na kuwaokoa wanyonge.
Katika kipindi hiki cha hatima, kusimama dhidi ya madhalimu na kuwasaidia waliodhulumiwa ni wajibu wa kidini na wa kibinadamu kwa watu wote huru duniani. Kwa msingi huo tunatangaza tena kuwa tutabaki kuwaunga mkono wanyonge duniani kote: kuanzia Palestina hadi Yemen, kutoka Lebanon na Syria hadi Myanmar na Venezuela.
Tunawaonya waziwazi madola ya kibeberu:
Vitu Vitakatifu vya Kiislamu na nafasi tukufu ya uongozi wa dini - ambayo leo inabebwa na Ayatullah al-Udhma Imam Khamenei (Mungu amlinde) - ni mstari wetu mwekundu wa hakika na wa maisha.
Ikiwa madhalimu wanajali kuendelea kuwepo kwao, basi wasithubutu hata kufikiria kuvamia heshima hii; vinginevyo watakutana na dhoruba ya ghadhabu takatifu yenye matokeo mabaya na yasiyotarajiwa.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atujalie ushindi wa mwisho wa kambi ya haki na umoja wa Umma wa Kiislamu.
Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlul-Bayt Uturuki (AHLADER)
Your Comment