Uturuki imetangaza rasmi kuwa imefungia anga lake kwa ndege za Israel, ikiwa ni pamoja na ndege ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, na haitatoa ruhusa yoyote kwa safari yake kwenda Azerbaijan. Hatua hii imechukuliwa kutokana na sera za utawala wa Israel kuhusu Gaza, na Uturuki inaendelea kuunga mkono haki za watu wa Palestina.
Kufuatia maandamano ya Uturuki yaliyotokana na kukamatwa kwa Meya wa Istanbul, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki ametangaza kukamatwa kwa watu 343 katika majimbo 9 ya nchi hiyo.
Hivi sasa, kuna hali (ihtimali) nne zinazowezekana kwa ajili ya mustakabali wa Akram Imam-oglu, Meya wa Istanbul na Mgombea anayetarajiwa katika uchaguzi wa Rais wa Uturuki.