6 Agosti 2025 - 22:02
Kuuawa na kujeruhiwa kwa Waislamu 5 wa Kishia nchini Pakistan katika shambulio la kundi la kitakfiri la Sipah-e-Sahaba

Waislamu wawili wa Kishia wameuawa shahidi katika shambulio la kigaidi lililotokea katika jiji la Karachi, Pakistan.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (as) – ABNA – vyanzo vya habari vimeripoti kuhusu shambulio la kigaidi dhidi ya kundi la Waislamu wa Kishia katika jiji la Karachi, jiji kubwa zaidi nchini Pakistan na mji mkuu wa Jimbo la Sindh.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wanachama wa kundi la kitakfiri la Sipah-e-Sahaba walishambulia kundi la Waislamu wa Kishia katika eneo la Pahlwan Goth ndani ya jiji la Karachi, ambapo mashambulizi hayo yalisababisha kuuawa shahidi kwa Waislamu wawili wa Kishia na kujeruhiwa kwa wengine watatu.

Waliouawa katika shambulio hilo ni Ali Waris mwana wa Rajab Ali Bangash, na Mazhar Abbas, huku walioumia wakiwa ni Ali Hassan, Muhammad Ali, na Habib Ali.

Inafaa kuashiria kuwa Sipah-e-Sahaba ni kundi kubwa zaidi la kitakfiri linalopinga Waislamu wa Kishia nchini Pakistan, lililoanzishwa mwaka 1985 na kundi la wanazuoni wa Kiwahabi likiongozwa na Haqq Nawaz Jhangvi huko Punjab, Pakistan. Kundi hili na tawi lake la kijeshi lijulikanalo kama Lashkar-e-Jhangvi limekuwa likiwakufurisha Waislamu wa Kishia na katika kipindi cha takribani miongo minne limekuwa na nafasi kubwa katika uchochezi wa ghasia za kimadhehebu na mashambulizi dhidi ya Waislamu wa Kishia nchini Pakistan na Afghanistan.

Vitendo vya kigaidi vya Sipah-e-Sahaba vimesababisha mara kadhaa serikali ya Pakistan kulipiga marufuku kundi hilo, huku viongozi wake watano wakiuawa katika mizozo ya kimadhehebu.

Kuuawa na kujeruhiwa kwa Waislamu 5 wa Kishia nchini Pakistan katika shambulio la kundi la kitakfiri la Sipah-e-Sahaba

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha