Waislamu
-
Kwa mujibu wa Qur'an Tukufu: Kundi la Mwenyezi Mungu, linalomtii Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na waliokuwa Waumini wa kweli, Hao ndio washindi wa kweli
"Hezbollah" humaanisha: Kundi lililojifunga na miongozo ya Mwenyezi Mungu, linalosimama na kutetea haki, hata likiwa ni dogo au linakabiliwa na maadui wakubwa. Aya hii imekuwa nembo ya Harakati za Muqawama (Upinzani wa Kiislamu) kama vile Hezbollah ya Lebanon, Ansarullah ya Yemen, na wengineo wanaopambana dhidi ya dhulma ya mabeberu ya Kimataifa.
-
Matendo Mema katika Dua na Swala za Sunna (Sehemu ya 1)
Huu ni mkusanyiko uliokusanya baadhi ya matendo ya kufanya usiku na mchana, swala za Sunnah zilizopokewa, ponyo, kinga, dhikir, dua za ajabu, athari za baadhi ya Aya na ufupisho wa kuwafanyia adabu waliokufa, nimezikusanya ili niziambatanishe kwenye Mafatihul Jinani kisha kitabu kikamilike kwa njia zote na iwe na manufaa kwayo yaliyotimia.
-
Ufafanuzi wa Kina na Maridhawa Juu ya Suala la Unabii Baina ya Waislamu na Wakristo
Sheikh Dk.Alhad Mussa Salum: "Wakristo wanaposema, au tunaposikia ikisemwa, au anapoitwa mtu kuwa ni Nabii au Nabii Mkuu, anaitwa hivyo kwa Istilahi ipi?! Hili ndio swali la msingi kujiuliza?. Anaitwa hivyo kwa Istilahi yetu sisi Waislamu au kwa istilahi yao hao ndugu zetu Wakristo?!. Kwa sababu katika suala la UNABII kila watu wana Istilahi zao".