Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Waduruze ni kundi la kidini la Kiarabu lenye historia ya usiri na itikadi za kipekee, linalopatikana hasa Syria, Lebanon na Palestina inayokaliwa. Ingawa baadhi ya watu wanawaona kama Waislamu, wengi wa waduruze hawajitambui hivyo, na mafundisho yao yanachanganya imani za Kiislamu, Kiyahudi, Kikristo na hata Kihindu.
Dini yao ilianza karne ya 11 chini ya ushawishi wa Hamza bin Ali na ikahusishwa na khalifa wa Fatwimiyah, al-Hakim bi Amrillah.
Wanaamini katika "Walii wa Zama" na kuzaliwa upya kwa roho (Tanasukh), huku mafundisho yao yakiwa ya siri, yakifundishwa kwa wachache tu miongoni mwao.
Jamii ya Kidruze ina mshikamano wa ndani, haifungamani kwa ndoa na watu wa nje wa dini yao, na inakataza talaka na mitala.
Katika siku za karibuni, kundi hili limeripotiwa kuhusika katika mauaji ya Waislamu huko Suwayda, Syria, kwa usaidizi wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel. Waduruze wanajulikana kuwa na uhusiano wa karibu na jeshi la Israel, ambapo vijana wao wengi wanahudumu humo.
Tukio hilo limeibua ghadhabu miongoni mwa Waislamu wa Syria waliolazimika kujibu mashambulizi hayo, lakini majeshi ya Kizayuni yakaingilia kuwalinda waduruze.
Kwa sasa, kundi hili linaonekana kutumiwa kama chombo cha kisiasa na kijeshi dhidi ya Waislamu katika eneo hilo, hasa katika mikakati ya Marekani na Israel ya kudhoofisha Umoja wa Ummah wa Kiislamu.
Your Comment