28 Oktoba 2025 - 22:56
Kutoka kwa Zainab al-Kubra(s) hadi leo; Karbala ni Chuo cha Habari cha Mwanamke Muumini /Wanawake Waislamu wako mstari wa mbele katika vita vya Habari

Misingi Mitatu ya Wajibu wa Mwanamke Mwislamu katika Ulimwengu wa Habari Kueneza uelewa: Mwanamke Mwislamu anapaswa kuwa sauti ya ukweli, afichue upotoshaji wa vyombo vya habari vya upande wa uongo, na atangaze mateso ya waliodhulumiwa duniani – kuanzia Palestina hadi kila sehemu inayokandamiza utu. Kutetea utambulisho: Vyombo vya habari vya kisasa vinajaribu kumvua mwanamke heshima yake na kumgeuza bidhaa ya matangazo. Mwanamke Mwislamu lazima athibitishe kuwa uhalisia na usasa vinaweza kuishi pamoja, na kwamba heshima hupimwa kwa utiifu wa ujumbe wa Mwenyezi Mungu, si kwa uchi au mvuto wa sura. Kulea kizazi cha waandishi wa kweli: Wajibu wa mwanamke hauishii katika kushiriki binafsi katika vyombo vya habari; anatakiwa kulea kizazi kinachotambua nguvu ya neno na dhamana ya uandishi wa ukweli.

Kutoka kwa Zainab al-Kubra(s) hadi leo; Karbala ni Chuo cha Habari cha Mwanamke Muumini /Wanawake Waislamu wako mstari wa mbele katika vita vya Habari

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Sambamba na maadhimisho ya kuzaliwa kwa bibi Zainab al-Kubra (a.s), kikao maalum chenye kichwa “Nafasi ya Wanawake katika Vyombo vya Habari vya Mapambano” kiliandaliwa katika makao makuu ya shirika hilo, kikihudhuriwa na wataalamu kutoka Lebanon na Syria.

Miongoni mwa wazungumzaji walikuwa:

1_Dkt. Qudwah Abdul-Sattar, mwandishi na mtafiti kutoka Lebanon,

2_Dkt. Linda Taboush, mhadhiri wa chuo kikuu na mtafiti kutoka Lebanon,

3_Dkt. Fatimah Azadi-Manesh, mtafiti na mwanahabari kutoka Syria.

Kutoka kwa Zainab al-Kubra(s) hadi leo; Karbala ni Chuo cha Habari cha Mwanamke Muumini /Wanawake Waislamu wako mstari wa mbele katika vita vya Habari

Dkt. Qudwah Abdul-Sattar: “Mwanamke Mwislamu si sauti iliyonyamazishwa”

Dkt. Abdul-Sattar alianza kwa kusema:
“Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliyelitukuza Uislamu kwa nuru ya ukweli na kuipa ubinadamu – wa kiume na wa kike – hadhi kupitia sauti na neno. Rehma na amani zimshukie Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt wake waliokuwa taa za uongofu.”

Alisisitiza kuwa katika historia ya Uislamu, mwanamke amekuwa mshiriki hai katika kueneza uelewa na kupinga dhulma. Akasema:
“Kutaja tu jina la Bibi Zainab (a.s) linatosha kuthibitisha hili. Alisimama imara mbele ya utawala wa kizayuni wa wakati huo – Yazid ibn Mu‘awiya – na kwa neno lake la haki alifichua sura ya dhulma. Aligeuza kushindwa kwa kijeshi kuwa ushindi wa milele wa kimaadili na kiuhabari.”

 “Vita vya leo ni vita vya habari”

Akasema:
“Nguvu ya mataifa leo haipimwi tena kwa mizinga na vifaru, bali kwa nguvu ya vyombo vya habari. Vyombo hivi vimekuwa silaha kuu ya ushawishi — vinapotosha ukweli, vinapamba uongo, na vinapanda mbegu za shaka katika nafsi za vijana. Lengo lao ni kuangamiza utambulisho, utamaduni na misingi ya mataifa.”

Hata hivyo, akaongeza:
“Hapa ndipo nafasi ya mwanamke Mwislamu inapodhihirika zaidi. Akiwa mwandishi, mwanablogu, mwalimu, au mlezi wa familia, anaweza kuwa sauti ya ukweli yenye nguvu zaidi ya risasi - kwani sauti hiyo inaingia katika akili na mioyo.”

Kutoka kwa Zainab al-Kubra(s) hadi leo; Karbala ni Chuo cha Habari cha Mwanamke Muumini /Wanawake Waislamu wako mstari wa mbele katika vita vya Habari

Misingi Mitatu ya Wajibu wa Mwanamke Mwislamu katika Ulimwengu wa Habari

  1. Kueneza uelewa:
    Mwanamke Mwislamu anapaswa kuwa sauti ya ukweli, afichue upotoshaji wa vyombo vya habari vya upande wa uongo, na atangaze mateso ya waliodhulumiwa duniani – kuanzia Palestina hadi kila sehemu inayokandamiza utu.

  2. Kutetea utambulisho:
    Vyombo vya habari vya kisasa vinajaribu kumvua mwanamke heshima yake na kumgeuza bidhaa ya matangazo. Mwanamke Mwislamu lazima athibitishe kuwa uhalisia na usasa vinaweza kuishi pamoja, na kwamba heshima hupimwa kwa utiifu wa ujumbe wa Mwenyezi Mungu, si kwa uchi au mvuto wa sura.

  3. Kulea kizazi cha waandishi wa kweli:
    Wajibu wa mwanamke hauishii katika kushiriki binafsi katika vyombo vya habari; anatakiwa kulea kizazi kinachotambua nguvu ya neno na dhamana ya uandishi wa ukweli.

“Tupambane kwa neno la uhuru”

Dkt. Abdul-Sattar alihitimisha:
“Tuseme kwa pamoja neno letu la uhuru, kwa jina la Mwenyezi Mungu na kwa utambulisho wetu wa asili, ili tuvunje miradi ya ukoloni na utawala wa kimfumo. Mwanamke Mwislamu ana nafasi ya kipekee katika mstari wa mbele wa mapambano haya, kama alivyokuwa daima katika historia ya ukweli.”

Kutoka kwa Zainab al-Kubra(s) hadi leo; Karbala ni Chuo cha Habari cha Mwanamke Muumini /Wanawake Waislamu wako mstari wa mbele katika vita vya Habari

Dkt. Linda Taboush: “Wanawake Waislamu wako mstari wa mbele katika uelewa na mapambano”

Dkt. Taboush alizungumzia ushiriki wa wanawake katika harakati za kijamii na kisiasa, akiwapongeza wanawake wa Palestina, Lebanon, na Iran kwa mchango wao mkubwa katika mapambano ya uelewa.

Akasema:
“Wanawake wa Iran tangu Mapinduzi ya Kiislamu hadi leo wamekuwa ngome thabiti ya mapambano. Vivyo hivyo wanawake wa Lebanon, tangu enzi za Imam Musa Sadr na Sayyid Abbas Moussawi hadi uongozi wa Sheikh Naeem Qassem, wamekuwa bega kwa bega na harakati za mapambano.”

Mwanamke ni kiini cha uelewa na marekebisho ya jamii

Alisema:
“Wanawake wanathibitisha uwepo wao kama nguvu ya ujenzi wa jamii, wanachangia katika kukuza fikra, utamaduni na maadili. Wanaifanya jamii iwe thabiti mbele ya changamoto.”

Akasisitiza kuwa utamaduni wa Magharibi umemchonganisha mwanamke na asili yake ya ki-Mungu, ukimvutia katika upotovu. Lakini Uislamu unamtazama mwanamke kama kiumbe mwenye jukumu la kufikia ukamilifu wa kiroho na kibinadamu - mfano bora ukiwa Zainab al-Kubra (a.s) na Umm Wahab, mwanamke wa kwanza kuuliwa shahidi katika Karbala.

 “Karbala ni chuo cha habari cha Mwanamke Muumini”

Akaendelea:
“Wanawake wa Karbala waliusambaza ujumbe wa haki duniani. Hata hivyo, bado hatujawatambulisha vya kutosha kama mifano ya wanawake hodari na waaminifu. Tunapaswa kuiga ujasiri na hekima zao.”

Kisha akamnukuu Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Khamenei:
“Wanawake wamekuwa uti wa mgongo wa mapinduzi na ulinzi wa taifa, na nafasi hiyo itaendelea kuwa muhimu.”

 “Uandishi wa habari ni utume, si ajira”

Akaongeza:
“Vyombo vya habari si uwanja wa umaarufu au biashara, bali ni jukumu la kiutu na kiimani. Mwanamke mwaminifu hatumii uzuri wake kutafuta kazi, bali hutumia akili, imani na maadili kueneza nuru ya ukweli.”

Dkt. Fatimah Azadi-Manesh: “Mwanamke Mwislamu wa leo ni mwandishi wa habari wa mstari wa mbele”

Dkt. Azadi-Manesh alisema:
“Magharibi imekosea kwa kudhani kuwa mwanamke Mwislamu amejificha nyuma ya hijabu. Ukweli ni kinyume chake — leo mwanamke ndiye nguvu inayoibeba jamii na harakati za mapambano.”

Mwanamke ni zaidi ya nusu ya jamii”

Akasema:
“Wanawake ni zaidi ya nusu ya jamii  - ni walezi, waalimu, dada, mama na viongozi wa fikra. Kwa kalamu, sauti na hata uwepo wao, wanapigania haki.”

Akaongeza:
“Kama isingekuwa Zainab (a.s), kusingekuwa na Karbala. Ni sauti yake iliyoupa uhai wa milele. Vivyo hivyo, leo Karbala inajirudia katika kila zama - wanawake lazima wajitambue katika uwanja huu wa mapambano.”

Kila mwanamke ni mwanahabari wa mapambano

Akasema:
“Katika zama hizi, kila mwanamke Mwislamu ni mwanahabari - hata anapotuma ujumbe wa haki kupitia picha au maneno machache mitandaoni. Yeye mwenyewe ni chombo cha habari, hata bila kamera au gazeti.”

 “Uandishi wa habari wa Kiislamu ni wa maadili”

Akasema:
“Tujifunze kutoka kwa Fatimah (a.s) na Zainab (a.s). Waliposema, walizungumza kwa hekima, heshima na maadili. Zainab alipozungumza katika kasri la Yazid, watu walisema: ‘Hii ni sauti ya binti wa Haidar.’ Hivyo ndivyo sura ya kweli ya vyombo vya habari vya Kiislamu inavyotakiwa kuwa.”

 “Uandishi wa habari ni uwanja wa imani na maadili”

Akaongeza:
“Tupambane kwa elimu, maadili na uongozi wa kimaadili wa Bibi Zahra (a.s) na Bibi Zainab (a.s). Huo ndio uso halisi wa vyombo vya habari vya mapambano. Na tunatumaini juhudi hizi zote zitabarikiwa kwa maombi ya Imam wetu, Sahib al-Zaman (a.f).”

Mwisho 
Kutoka Karbala hadi leo, mwanamke Mwislamu ndiye mhimili wa mawasiliano ya haki, akibeba ujumbe wa uelewa, heshima na imani. Sauti ya mwanamke muumini – inapozungumza kwa ukweli – ni silaha yenye nguvu kuliko risasi.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha