Mwandishi
-
Katika Kikao cha "Nafasi ya Wanawake wa Vyombo vya Habari katika Muqawama (Mapambano - Upinzani) ilibainika:
Kutoka kwa Zainab al-Kubra(s) hadi leo; Karbala ni Chuo cha Habari cha Mwanamke Muumini /Wanawake Waislamu wako mstari wa mbele katika vita vya Habari
Misingi Mitatu ya Wajibu wa Mwanamke Mwislamu katika Ulimwengu wa Habari Kueneza uelewa: Mwanamke Mwislamu anapaswa kuwa sauti ya ukweli, afichue upotoshaji wa vyombo vya habari vya upande wa uongo, na atangaze mateso ya waliodhulumiwa duniani – kuanzia Palestina hadi kila sehemu inayokandamiza utu. Kutetea utambulisho: Vyombo vya habari vya kisasa vinajaribu kumvua mwanamke heshima yake na kumgeuza bidhaa ya matangazo. Mwanamke Mwislamu lazima athibitishe kuwa uhalisia na usasa vinaweza kuishi pamoja, na kwamba heshima hupimwa kwa utiifu wa ujumbe wa Mwenyezi Mungu, si kwa uchi au mvuto wa sura. Kulea kizazi cha waandishi wa kweli: Wajibu wa mwanamke hauishii katika kushiriki binafsi katika vyombo vya habari; anatakiwa kulea kizazi kinachotambua nguvu ya neno na dhamana ya uandishi wa ukweli.
-
Mwandishi wa Kizayuni: Hamas bado ipo hai
"Wapiganaji wa Hamas wameonekana hadharani wakiwa wamevaa sare za kijeshi, jambo linalotoa ujumbe wazi kwa wale wote waliodhani kuwa vita vya miaka miwili vya Israel dhidi ya Hamas viliiangamiza, kwamba dhana hiyo imekuwa si sahihi, kwani Hamas imerejea tena kwa nguvu kwenye uwanja wa mapambano".
-
Ustahimilivu wa waandishi wa habari wa Yemen kutoka Sana'a hadi Gaza:
Kuanzia kwa kuuawa shahidi kwa waandishi wa habari 32 wa Kiyemeni hadi kusimama imara kwa mwandishi wa Al-Masirah chini ya mashambulizi ya mabomu Gaza
Waandishi wa habari wa Kiyemeni walipaa (walipata shahada) wakiwa wamesimama imara katika 'uwanja wa maneno', wakikabiliana na adui na 'mradi wa uharibifu wa uvamizi wa kimataifa' unaoongozwa na Marekani, hadi wakapata shahada.
-
Mtazamo juu ya Septemba ya Umwagaji Damu Lebanon;Kuanzia Jinai za Pagers hadi Subira ya Kistratejia ya Hizbullah baada ya Shahidi “Sayyid wa Muqawama"
Siku hizi ni kumbukumbu ya jinai za kipekee za utawala wa Kizayuni nchini Lebanon – kuanzia milipuko ya pageri hadi mauaji ya makamanda waandamizi wa Hizbullah. Hivyo basi, Septemba ya mwaka uliopita kwa Wana-Lebanon imekuwa mwezi usiosahaulika
-
-
Pezeshkian: Jibu la ujasiri la Mwanahabari wa Kike (Simba Jike) wa Iran lilikuwa ishara ya uthabiti wa Taifa Imara la Iran
Pezeshkiani, alipongeza hatua ya mwandishi huyo wa habari wakati wa matangazo ya moja kwa moja akisema: "Maitikio ya kupongezwa ya simba jike huyu wa Iran kwenye kipindi cha moja kwa moja cha televisheni ni ishara ya upinzani (Muqawamah), uthabiti na kutoweza kushindwa kwa taifa lenye ustaarabu wa muda mrefu dhidi ya kelele za utawala usiojulikana asili yake na usio na sura halali."
-
Raundi ya Nne ya Mazungumzo kati ya Iran na Marekani Kufanyika Jumatano, Mei 7, 2025
Kwa mujibu wa Mwandishi wa Wall Street Journal, muda unaotarajiwa kwa ajili ya mazungumzo yajayo ni tarehe 7 Mei, 2025 (Siku ya Jumatano).