Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Anas al-Sharif, Mwandishi Mashuhuri wa Al Jazeera mwenye umri wa miaka 28 ambaye alikuwa akiripoti kutoka Kaskazini mwa Gaza, ameuawa pamoja na wenzake wanne katika shambulio la Israel dhidi ya mahema ya waandishi wa habari karibu na hospitali ya al-Shifa, Gaza.
Shambulio hili limelalamikiwa vikali na Al Jazeera kama ukatili wa kusababisha kuminya uhuru wa vyombo vya habari. Tukio hili linaashiria hatari kubwa inayowakumba waandishi wa habari katika maeneo ya mizozo.
Mwandishi wa Al Jazeera Anas al-Sharif na wenzake wanne wauawa katika shambulio la Israel Gaza
Your Comment