Hafla hii ya kiroho imehudhuriwa na talaba / Wanafunzi pamoja na walimu wa Hawza na inalenga kukuza maadili ya Kiislamu, kuimarisha ibada, na kuongeza mapenzi na mshikamano kupitia kukaa pamoja chini ya kivuli cha Qur’ani Tukufu.

18 Desemba 2025 - 23:56

Malawi | Hafla ya Usomaji wa Qur’an Tukufu +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kwa idhini na Tawfiq ya Mwenyezi Mungu, hafla tukufu ya usomaji wa Qur’ani Tukufu imeandaliwa kufanyika siku ya 18/12/2025, katika Msikiti (Swala) wa Shule ya Al-Hadi (as), mara baada ya Swala ya Adhuhuri na Alasiri.

Katika mkusanyiko huu wa baraka, talaba mpendwa Parshas Doba atasoma aya tukufu za Qur’ani kwa sauti nzuri na unyenyekevu mkubwa, ili kuimarisha uhusiano wa wanafunzi na walimu na Kitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungu, na kueneza nuru ya Qur’ani katika mazingira ya elimu na malezi.

Malawi | Hafla ya Usomaji wa Qur’an Tukufu +Picha

Hafla hii ya kiroho imehudhuriwa na talaba / Wanafunzi pamoja na walimu wa Hawza, na inalenga kukuza maadili ya Kiislamu, kuimarisha ibada, na kuongeza mapenzi na mshikamano kupitia kukaa pamoja chini ya kivuli cha Qur’ani Tukufu.

Malawi | Hafla ya Usomaji wa Qur’an Tukufu +Picha

Mikusanyiko ya aina hii ina mchango mkubwa katika kujenga malezi ya kiroho, kuimarisha nidhamu na maadili, na kuifanya Qur’ani kuwa sehemu hai ya maisha ya kila siku ya wanafunzi na walimu wa Shule ya Al-Hadi. Mwenyezi Mungu aijaalie hafla hii iwe chanzo cha kheri, baraka na mafanikio kwa wote watakaoshiriki.

Malawi | Hafla ya Usomaji wa Qur’an Tukufu +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha