Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt(a.s) – ABNA – Mwandishi wa Wall Street Journal, Laurence Norman, ametangaza kupitia mfululizo wa machapisho katika mtandao wa X kwamba: “Nimeambiwa kuwa mazungumzo yamepangiwa kufanyika tarehe 7 Mei, 2025 (Jumatano).” Katika chapisho jingine, alieleza kuwa tarehe hiyo bado si rasmi kwani inaonekana kuwa Wamarekani walihitaji muda zaidi.
Ni vyema kutaja kuwa saa chache kabla, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alitangaza kwamba raundi ijayo ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani, ambayo yalipangwa kufanyika Mei 2, 2025 mjini Roma, yameahirishwa.
Your Comment