Nyuklia
-
Araghchi: "Kiongozi Mkuu ameweka wazi wajibu wa Iran kuhusu urani na kwamba suala la urutubishaji wa Urani (uranium enrichment) halipo mezani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqhchi, alizungumza kuhusu msimamo wa Marekani katika mazungumzo ya nyuklia na kusisitiza kwamba suala la urutubishaji wa urani (uranium enrichment) halipo kabisa katika meza ya majadiliano. Alisema kuwa urutubishaji si jambo ambalo linapaswa kujadiliwa, kwani haki ya Iran ya kuendeleza mpango wake wa nyuklia ni jambo la msingi na lililowekwa wazi. Aidha, aliongeza kuwa: Kiongozi Mkuu alisema wazi kuhusu hili katika majadiliano yaliyopita na hakubali kuona suala hili likiingizwa tena katika mchakato wa majadiliano.
-
Kauli ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu wa Iran:
"Wamarekani waache kupayuka; Iran haitasubiri ruhusa ya mtu yeyote ili kuendeleza shughuli zake za kurutubisha urani"
Kiongozi wa Mapinduzi alipozungumzia mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Wamarekani, alisisitiza kuwa: Kauli ya Wamarekani kwamba 'hawataruhusu Iran irutubishe urani' ni upuuzi mtupu. Hakuna mtu yeyote nchini anayesubiri ruhusa ya huyu au yule. Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kufuata sera na njia yake kama kawaida.
-
Raundi ya Nne ya Mazungumzo kati ya Iran na Marekani Kufanyika Jumatano, Mei 7, 2025
Kwa mujibu wa Mwandishi wa Wall Street Journal, muda unaotarajiwa kwa ajili ya mazungumzo yajayo ni tarehe 7 Mei, 2025 (Siku ya Jumatano).