29 Juni 2025 - 15:07
Mchambuzi wa Kiyahudi: "Kwa Nini Tumeshindwa Vita na Iran Imeshinda Vita?"

Mchambuzi huyu wa Kiyahudi, Goldberg alisisitiza zaidi kuwa Makombora ya Iran yalilenga kwa usahihi mno Shabaha zake, na yameibuka kwa heshima kubwa kimataifa. Badala ya kusambaratika, Iran imeonekana kuwa Taifa thabiti na lenye msimamo wa kupambana na uonevu wa yeyote.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Ori Goldberg, Mchambuzi wa kisiasa wa Kiyahudi anayeishi Tel Aviv, ameandika tathmini kuhusu kushindwa kwa "Israel" katika mashambulizi yake dhidi ya Iran. Katika tathmini yake, aligusia malengo mawili yaliyotangazwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu mwanzoni mwa mashambulizi hayo.

Mchambuzi wa Kiyahudi: "Kwa Nini Tumeshindwa Vita na Iran Imeshinda Vita?"

Malengo hayo yaliyotajwa na Netanyahu ni haya yafuatayo:

Lengo la kwanza: Kuharibu mpango wa nyuklia wa Iran 

Hata hivyo, mpango huo wa Nyuklia wa Iran haukuharibika bali bado unaendelea. Wakati Marekani inashambulia vituo vya Nyuklia vya Iran, Iran ilikuwa tayari imehamisha vifaa muhimu vya kinyuklia kutoka vituo vyake muhimu kama Fordo na vingine kabla ya kushambuliwa.

Lengo la Pili: Kuing'oa Serikali ya Kiislamu

Hakuna lengo la Kisiasa wala kijeshi lililofikiwa. Dunia haikuunga mkono uvamizi wa "Israel," bali imeiona Iran kama mhanga wa dhulma.

Mchambuzi huyu wa Kiyahudi, Goldberg alisisitiza zaidi kuwa Makombora ya Iran yalilenga kwa usahihi mno Shabaha zake, na yameibuka kwa heshima kubwa kimataifa. 

Badala ya kusambaratika, Iran imeonekana kuwa Taifa thabiti na lenye msimamo wa kupambana na uonevu wa yeyote.

Aidha, alisema kuwa Iran haijashinda tu kijeshi, bali pia kimkakati na kiitikadi. 

Katika kivuli cha vita, utawala wa Kizayuni umepoteza heshima, kuungwa mkono kimataifa, na umeonyesha udhaifu mkubwa wa ndani. 

Mchambuzi wa Kiyahudi: "Kwa Nini Tumeshindwa Vita na Iran Imeshinda Vita?"

Netanyahu akionyesha jengo muhimu la Kisayansi la Israel la Taasisi ya Weizaman (Weizmann Institute of Science) lililopo katikati ya Mji wa Rehovot, ambapo Iran ililishambulia na kulifanya kuwa majivu kwa Kombora lenye tani moja, lililoharibu kikamilifu Taasisi hiyo ndani ya sekunde 7 tu, na Utafiti wote wa Kisayansi wa Kizayuni uliofanywa kwa muda wa miaka 70 ukaangamia. Hawakutegemea pigo kubwa kama hilo pindi walipochukua maamuzi ya kuichokoza Iran, walidhani Iran itawajibu kwa busara lakini wakajibiwa kwa kichapo kikubwa hawakuwahi kuona.

Tukirudi katika Uchambuzi wa Muyahudi bwana Goldberg, Mwisho anatoa: Tathmini yake ambayo inabainisha jinsi ambavyo Iran imeweza kudumisha msimamo wake na kuimarisha heshima yake kimataifa, wakati "Israel" inakabiliwa na matokeo mabaya kutokana na hatua zake za kijeshi zilizofeli dhidi ya Iran.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha