Msimamo
-
Kabla ya kuondoka Tehran kuelekea Iraq na Lebanon;
LariJani: Mkataba wa usalama kati ya Iran na Iraq unaandaliwa / Kusisitiza umoja wa kitaifa wa Lebanon
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa alisema kwamba usalama wa Iran unategemea usalama wa majirani zake na kuongeza: “Mkataba wa usalama kati ya Iran na Iraq unaandaliwa na utaasainiwa katika safari hii.”
-
Mchambuzi wa Kiyahudi: "Kwa Nini Tumeshindwa Vita na Iran Imeshinda Vita?"
Mchambuzi huyu wa Kiyahudi, Goldberg alisisitiza zaidi kuwa Makombora ya Iran yalilenga kwa usahihi mno Shabaha zake, na yameibuka kwa heshima kubwa kimataifa. Badala ya kusambaratika, Iran imeonekana kuwa Taifa thabiti na lenye msimamo wa kupambana na uonevu wa yeyote.
-
Araghchi: "Kiongozi Mkuu ameweka wazi wajibu wa Iran kuhusu urani na kwamba suala la urutubishaji wa Urani (uranium enrichment) halipo mezani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqhchi, alizungumza kuhusu msimamo wa Marekani katika mazungumzo ya nyuklia na kusisitiza kwamba suala la urutubishaji wa urani (uranium enrichment) halipo kabisa katika meza ya majadiliano. Alisema kuwa urutubishaji si jambo ambalo linapaswa kujadiliwa, kwani haki ya Iran ya kuendeleza mpango wake wa nyuklia ni jambo la msingi na lililowekwa wazi. Aidha, aliongeza kuwa: Kiongozi Mkuu alisema wazi kuhusu hili katika majadiliano yaliyopita na hakubali kuona suala hili likiingizwa tena katika mchakato wa majadiliano.