Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-: Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu wa Iran, asubuhi ya leo katika kikao na familia za Shahidi Rais Ebrahim Raisi na mashahidi wengine wa huduma, pamoja na familia za Mashahidi waliokuwa viongozi katika miongo ya hivi karibuni, alieleza kuwa: Lengo kuu la kuheshimu na kuwasifu Mashahidi ni kutafakari na kujifunza kutoka kwao.
Katika maelezo yake kuhusu sifa za moyo, kauli na vitendo vya Raisi, alisema:
"Raisi mpendwa alikuwa mfano kamili wa sifa za Kiongozi katika Serikali ya Kiislamu."
Aidha, aliongeza kuwa:
"Kwa jitihada zisizo na kuchoka, alilitumikia taifa, heshima, na hadhi ya watu. Njia na mtindo wake wa maisha ni funzo kubwa kwa viongozi wote, vijana, na vizazi vijavyo."
Kiongozi Mkuu, Ayatollah Khamenei, katika mkutano na familia za mashahidi wa huduma akiwemo Rais Shahidi Ebrahim Raisi, Shahidi Al-Hashem, Shahidi Amir-Abdollahian, mashahidi wa kikundi cha safari ya anga, Gavana wa Azarbaijan ya Mashariki, na Kamanda wa Ulinzi, aliwapongeza kwa kujitolea kwao na akatoa mafunzo kadhaa muhimu:
Msimamo kuhusu Marekani na urutubishaji wa urani:
Ayatollah Khamenei alisisitiza kwa mara nyingine kuwa:
Kauli ya Wamarekani kwamba ‘hawataruhusu Iran irutubishe urani’ ni upuuzi usiovumilika.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kufuata sera yake ya kujitegemea bila kusubiri ruhusa ya yeyote.
Sifa za Rais Shahidi Raisi:
Ayatollah Khamenei alimwelezea Raisi kama:
-
Mfano kamili wa Kiongozi wa Serikali ya Kiislamu.
-
Mtu wa moyo mnyenyekevu (khushuu’), lugha ya ukweli na uaminifu, na vitendo visivyochoka.
-
Aliwatumikia watu kwa uadilifu, bila kujinufaisha na nafasi ya kisiasa.
-
Aliamini kuwa yeye ni miongoni mwa watu, na wakati mwingine hata mdogo kuliko wao.
-
Hakuwahi kulalamika au kuwa na dhana mbaya juu ya watu, bali aliendelea kuhofia kutotekeleza vyema majukumu yake.
Kinyume cha Serikali za Kifirauni:
Kwa kuzingatia aya za Qur’ani, Kiongozi Mkuu alisema:
Sifa za serikali ya kifirauni ni kama kujiona bora, kuwadharau watu, na kuwabebesha majukumu yao.
Raisi, alisema, alikuwa kinyume kabisa cha haya – alikuwa mnyenyekevu, mwenye huruma, na mwenye kujitolea.
Mafunzo kwa Viongozi na Jamii:
Ayatollah Khamenei alisema:
-
Watu wengi ndani ya mfumo wa Kiislamu wana sifa kama za Raisi, lakini ni muhimu sifa hizi ziwe utamaduni wa jamii nzima.
-
Lengo pekee la Raisi katika kuongoza Idara ya Mahakama na kushiriki uchaguzi wa Rais, lilikuwa ni kutekeleza wajibu wa kidini (taklīf).
-
Watu wengi husema wanatekeleza wajibu, lakini kwa Raisi, tuliliona suala hilo kwa vitendo.
Lugha ya Raisi Shahidi katika siasa na diplomasia:
Kiongozi Muadhamu alisema kuwa:
Lugha ya Shahidi Raisi, ndani ya nchi na hata katika medani ya diplomasia, ilikuwa ya uwazi na ukweli.
Alisimama kidete katika misimamo yake na hakuruhusu maadui kudai kwamba Iran imeletwa kwenye meza ya mazungumzo kwa hila, vitisho au ahadi za tamaa.
Msimamo Kuhusu Mazungumzo ya Moja kwa Moja:
Ayatollah Khamenei alieleza kuwa:
Lengo la upande wa pili (Marekani) katika kushinikiza yawepo mazungumzo ya moja kwa moja ni kuonyesha kwamba Iran imejisalimisha.
Raisi hakuwapa fursa hiyo.
Mazungumzo ya moja kwa moja hayakufanyika, bali ya moja kwa moja yalifanyika kama sasa, lakini hayakufanikisha chochote, na hata sasa hatutarajii matokeo — hatujui yatakuwaje.
Kauli dhidi ya Marekani Kuhusu Urutubishaji:
Ayatollah Khamenei alisisitiza:
Kauli ya Wamarekani kwamba ‘hawataruhusu Iran irutubishe urani’ ni upuuzi mkubwa.
Hakuna mtu yeyote nchini anayesubiri ruhusa ya yeyote.Iran itaendelea na sera yake kama kawaida.
Aliongeza kuwa:
Katika wakati mwafaka (kwenye mnasaba wowote ujao), atawaambia watu wa Taifa la Iran ni kwa nini Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi wanasisitiza sana kwamba Iran isifanye urutubishaji wa nyuklia.
Ukweli wa Raisi vs. unafiki wa Magharibi:
Ayatollah Khamenei alisema:
Ukweli na uwazi wa Raisi unaweza kulinganishwa na uongo wa viongozi wa baadhi ya nchi za Magharibi, ambao:
-
Hudai kutetea Amani na Haki za Binadamu,
-
Lakini wamefumba macho kwa mauaji ya zaidi ya watoto 20,000 wasio na hatia huko Gaza,
-
Na hata wanawasaidia wahalifu hao wa Kizayuni (kuendelea kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu madhulumu wa Palestina).
Bidii ya Kazi na Huduma kwa Wananchi:
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, alimwelezea Shahidi Raisi kama:
-
Mfano wa Kiongozi aliyejitolea kikamilifu.
-
Hakuwa na uchovu, hakujali mchana wala usiku.
-
Alipoambiwa apunguze kazi ili alinde afya, alijibu:
-
“Mimi sichoki kufanya kazi.”
Aliyataja mafanikio ya Raisi kuwa ni kama vile:
-
Mradi wa maji vijijini na mijini,
-
Ujenzi wa barabara,
-
Kuunda ajira,
-
Kufufua viwanda vilivyokufa,
-
Kukamilisha miradi iliyokwama.
Alisema kuwa Raisi alitumikia watu kwa njia ya moja kwa moja na inayogusika (na kuonekana kwa macho), na pia alitetea heshima, utu na hadhi ya Taifa la Iran kwa kiwango cha juu.
Ongezeko la Uchumi wa Iran:
Ayatollah Khamenei alikubali na kusema:
Ripoti kutoka kwa vituo vya kifedha vya kimataifa inadhihirisha ongezeko la uchumi wa Iran kutoka karibu sifuri mwanzoni mwa utawala wa serikali ya 13 hadi karibu asilimia 5 mwishoni mwa utawala huo.
Hii ni fahari na heshima kubwa kwa taifa la Iran, na ni ishara ya maendeleo ya taifa.
Aliongeza kuwa:
Kuinua Qur’ani au picha ya Shahidi Soleimani kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni baadhi ya hatua ambazo Shahidi Raisi alichukua ili kuliinua na kulitukuza taifa la Iran.
Msingi wa Maadili ya Kiongozi wa Kiislamu:
Ayatollah Khamenei aliendelea kusema kwamba:
Kuonyesha mwanga, roho, motisha, na hisia za kuwajibika kwa viongozi vijana wa Mapinduzi ya Kiislamu (kama vile wenzake wa Shahidi Rajai) ni mfano wa nguvu za Mapinduzi ya Kiislamu.
Tunaendelea kuzalisha viongozi waliojitolea na wenye ufanisi, na hili ni ushindi wa Mapinduzi yaliyofanywa na Imam Khomeini (M.A).
Uwezeshaji wa Vijana na Maendeleo ya Mapinduzi:
Ayatollah Khamenei alisisitiza:
Mashahidi wa ajali ya ndege ya Mei walikuwa ama vijana au watoto ambao hawakuwa wamezaliwa wakati wa Mapinduzi ya Kiislamu. Hii ni ishara ya nguvu za Mapinduzi ya Kiislamu; Mapinduzi haya yana uwezo wa kuhamasisha vijana kama Arman Ali-Vardi, kijana mwenye umri wa miaka 19, na kumweka katika mstari ule ule ambao Shahidi Ayatollah Ashrafi Isfahani, mwenye umri wa miaka 90, aliaga dunia akipigania Taifa.
Alisema:
Huu ni uthibitisho wa nguvu ya Mapinduzi ya Kiislamu, ambayo inatoa uwezo wa kuhamasisha na kuunganisha nguvu za vijana.
Nguvu ya Mapinduzi ya Kiislamu:
Ayatollah Khamenei aliongeza:
Mapinduzi haya, yaliyobarikiwa na uwezo huu wa kuhamasisha vijana kwa nguvu, hayawezi kushindwa. Tunapaswa kuthamini Mapinduzi haya, uwezo wake wa kuzalisha viongozi bora, maendeleo yaliyopatikana, na harakati kubwa ya taifa la Iran. Tunapaswa kuomba msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili Mapinduzi haya yaendelee, na kuwa mfano wa kudumu kwa taifa la Iran, na kwa mataifa mengine duniani.
Mwisho wa Kunukuu.
Tanbihi:
Maneno hayo katika Hotuba hii yanadhihirisha na kusisitiza kuwa Mapinduzi ya Kiislamu yameweza kuzalisha viongozi wa kiadilifu, walio na motisha na uwezo wa kufanya mabadiliko makubwa katika jamii, na kwamba kiini cha mafanikio haya ni kuendelea na umoja wa kitaifa na imani ya kidini.
Your Comment