Katibu wa Kwanza wa Kongamano la Kimataifa la Mfano wa Uongozi wa Shahid Ayatollah Dkt. Sayyid Ebrahim Raisi: Kongamano Limekuwa Jukwaa la Kimataifa kwa Ufafanuzi wa Uongozi wa Kiislamu
Katibu wa kongamano la kwanza la kimataifa kuhusu mfano wa uongozi wa Shahid Ayatollah Dkt. Sayyid Ebrahim Raisi amesema kuwa, kongamano hili limekuwa jukwaa la kimataifa kwa ajili ya kufafanua dhana ya uongozi wa Kiislamu, kupitia vikao mbalimbali vilivyofanyika katika nchi sita — ambazo ni India, Pakistan, Indonesia, Malaysia, Iraq na Iran.
Kiongozi wa Mapinduzi alipozungumzia mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Wamarekani, alisisitiza kuwa: Kauli ya Wamarekani kwamba 'hawataruhusu Iran irutubishe urani' ni upuuzi mtupu. Hakuna mtu yeyote nchini anayesubiri ruhusa ya huyu au yule. Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kufuata sera na njia yake kama kawaida.