Mashahidi
-
Sheikh Naeem Qassem:
"Kulenga Palestina, Muqawama na Iran ni sehemu ya vita moja / Mpango hatari wa Trump kwa Gaza: Vazi la Kimarekani juu ya mpango wa Kizayuni"
Katibu Mkuu wa Hizbullah nchini Lebanon, Sheikh Naeem Qassem, katika maadhimisho ya mwaka mmoja wa shahada ya mashujaa wawili wa muqawama — Shahid Sheikh Nabil Qawuq na Sayyid Suhail Al-Husseini — alionya kuhusu sura mpya ya mradi wa Kizayuni unaoitwa “Israel Kubwa” na kusisitiza juu ya kuendelea kwa mapambano na ulinzi wa mhimili wa haki.
-
Shahidi aliyekuwa akiishi kwa Mashahidi | Simulizi la Mama wa Shahidi kuhusu wakati wa mlipuko na Shahada
moja kwa mzaha nilimwambia mwanangu “Mwanangu! Kwa nini unanibana sana kuhusu kusali kwa wakati?” Alitabasamu na kusema: «Mama! Ninaogopa tufariki bila kusali kwa wakati na tusipate nafasi ya kurekebisha...»
-
Idadi ya Mashahidi wa Gaza yafikia 64,803
Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa jumla ya mashahidi katika eneo hilo imefikia watu 64,803.
-
Ujumbe wa Rambirambi kutoka kwa Ayatullah Dori Najafabadi kwa Watu wa Yemen: "Ushujaa wa Mashahidi Utaimarisha Umoja Dhidi ya Adui wa Kizayuni"
Ninawapa pole familia za mashahidi hawa wapendwa na wananchi wote wa Yemen. Tunawakumbuka mashahidi wote wa Uislamu: kuanzia mashahidi wa tukio la Fakh, mashahidi wa Palestina, Lebanon, na mashahidi wetu wa Iran kama vile Shahidi Qassem Soleimani na wengine.
-
Zaidi ya Vikundi 200 vya Maombolezo vya Watu wa Mazandaran Wakiwa kwenye Haram ya Imam Ridha (a.s) / Mila ya Kihistoria ya Waombolezaji wa Kaskazini
Mkurugenzi wa Idara ya Tablighat Islami ya Mazandaran amesema: Mwaka huu zaidi ya vikundi 200 vya maombolezo kutoka miji mbalimbali ya mkoa huu, kwa hisia na ufahamu wa kipekee, vimeshiriki kwenye hafla za maombolezo na mikusanyiko ya kidini katika Haram ya Imam Ridha (a.s), na hivyo mila ya kihistoria ya watu wa Mazandaran imefanyika tena kwa upeo mkubwa.
-
Kuongezeka kwa Idadi ya Mashahidi wa Njaa Gaza hadi 269
Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa katika saa 24 zilizopita watu wengine watatu wamepoteza maisha yao kutokana na njaa na ukosefu wa chakula.
-
Dkt. Larijani: Sayyid Hassan Nasrallah alikuwa hazina kubwa kwa ulimwengu wa Kiislamu
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika ziara yake kwenye eneo la Dahieh Kusini mwa Beirut na kutembelea kaburi la Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, alimueleza kuwa ni hazina kubwa kwa ulimwengu wa Kiislamu na kusisitiza juu ya kuendeleza njia ya muqawama (upinzani wa haki).
-
Magharibi mwa Asia na Mashariki ya Kati | Watu 11 Wauawa na Kujeruhiwa Kutokana na Mlupuko wa Mabomu Yaliyosalia huko Tyre, Lebanon
Watu 11 wa jeshi la Lebanon wameuawa na kujeruhiwa kufuatia mlipuko wa mabomu yaliyosalia kutoka kwenye uvamizi wa awali wa utawala wa Kizayuni kusini mwa Lebanon, tukio ambalo limepelekea viongozi wa juu wa nchi hiyo kutuma salamu za rambirambi.
-
Washairi wa Kimataifa Waungana na Washairi wa Iran Kuadhimisha Mashahidi katika Usiku wa Mashairi ulioitwa: “Wasafiri wa Alfajiri”
Katika hafla hii, washairi walitumia lugha ya fasaha na yenye kugusa hisia kueleza hadhi ya mashahidi, wakisoma mashairi yenye maudhui ya hisia, ujasiri na ucha Mungu, ambayo yalionyesha sio tu upendo wa kibinadamu bali pia dhamira ya kijamii, mwamko wa kiutamaduni na mshikamano wa kitaifa.
-
Siku ya 11 baada ya A'shura | Karbala imetenganisha Kati ya Dini ya Kuabudu Matwaghuti (Bani Umaiyya) na Dini ya Kumuabudu Mwenyezi Mungu
Dini ya Kumuabudu Mwenyezi Mungu (swt) baada ya vita vya Karbala iliwakilishwa na damu ya Imam Hussein (a.s) na Mashahidi wa Karbaka ambayo ilikuwa kielelezo hai cha dini ya haki ya Mwenyezi Mungu.
-
Wayahudi Wanaopinga Uzayuni Wametoa Pongezi kwa Mashahidi wa Mashambulizi ya Israel Dhidi ya Iran
Mayahudi wanao uchukia Uzayuni huko New York, walihudhuria katika Ofisi ya Ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa mjini New York na kutoa heshima zao kwa Mashahidi wa Mashambulizi ya Utawala wa Kizayuni.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran:
"Kila afisa wa Kijeshi au Mwanasayansi wa Nyuklia wa Iran anayeuliwa Kigaidi, kuna wengine mia moja nyuma yake walioko tayari kuchukua nafasi yake"
Abbas Araqchi alisema: "Tofauti na utawala wa Kizayuni, Iran haitaficha kamwe hasara zake na inajivunia Mashahidi wake kama vielelezo vya ujasiri. Taifa la Iran litasimama kidete dhidi ya yeyote anayejaribu kuliamulia mustakabali wake hadi tone la mwisho la damu".
-
Wito kwa wananchi wa kushiriki kwa wingi kwenye mazishi ya Mashahidi wa Mamlaka ya ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Baraza la Uratibu wa Propaganda (Tablighi) za Kiislamu limetoa taarifa na kutangaza: Marasimu ya mazishi ya miili mitukufu ya mashahidi wa ngazi za juu kuwa itafanyika siku ya Jumamosi tarehe 27 Julai 2025, saa 8:00 Asubuhi mbele ya Chuo Kikuu cha Tehran.
-
Mkuu wa Shirika la ujasusi la IRGC na Naibu wake Waliuawa Shahidi
Walinzi wa Mapinduzi walitoa taarifa na kutangaza kuuawa Shahidi Mkuu wa upelelezi Mohammad Kazemi na naibu wake.
-
Tangazo kutoka kwa Baraza la Uratibu wa Propaganda za Kiislamu:
Marasimu ya Mazishi ya Miili Mitukufu ya Mashahidi wa Walinzi na Watetezi wa ngazi za juu wa Iran ya Kiislamu itafanyika
Baraza la Uratibu wa Propaganda za Kiislamu limetangaza katika taarifa yake kwamba, hafla ya mazishi ya miili mitukufu ya mashahidi wa ngazi za juu ambao ni walinzi na watetezi wa Iran ya Kiislamu itafanyika Siku ya Jumanne, tarehe 17 Juni, 2025, saa 8:00 Asubuhi katika Medani ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Tehran.
-
Waathirika wa mlipuko wa vipiga simu vya pager nchini Lebanon Washiriki katika uchaguzi nchini Lebanon
Waathirika wa mlipuko wa vipiga simu vya pager nchini Lebanon walishiriki katika awamu ya nne ya uchaguzi wa madiwani wa manispaa (na mitaa) katika maeneo ya kusini mwa Lebanon na kuweka kura zao kwenye sanduku la kupigia kura. Hii ni hatua muhimu ya kushiriki kidemokrasia kwa waathirika hawa ambao wanatumia sauti yao kuleta mabadiliko katika jamii zao.
-
Kauli ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu wa Iran:
"Wamarekani waache kupayuka; Iran haitasubiri ruhusa ya mtu yeyote ili kuendeleza shughuli zake za kurutubisha urani"
Kiongozi wa Mapinduzi alipozungumzia mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Wamarekani, alisisitiza kuwa: Kauli ya Wamarekani kwamba 'hawataruhusu Iran irutubishe urani' ni upuuzi mtupu. Hakuna mtu yeyote nchini anayesubiri ruhusa ya huyu au yule. Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kufuata sera na njia yake kama kawaida.
-
"Kutoka 'Juhudi Zisizoisha' hadi kwenye 'Diplomasia ya Muqawamah'; Wiki ya Kuwapa Heshima Mashahidi wa Huduma"
"Saeed Ohadi, Mkuu wa Kamati ya Maadhimisho ya Kumkumbuka Shahidi Ayatollah Sayyid Ebrahim Raisi na Mashujaa wengine wa Huduma, ameeleza kwa kina ratiba ya maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka wa kwanza ya mashahidi wa huduma."
-
Nyuma ya Pazia la Uhalifu wa Vyombo vya Habari: Kumvunjia heshima Sayyid wa Mashahidi wa Muqawama kupitia Kituo kimoja cha Televisheni cha Kilebanon
Hivi karibuni, televisheni ya Al-Jadeed ilirusha ripoti kutoka kwenye Kaburi la Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, ambapo ilitoa matamshi ya matusi dhidi ya shahidi huyu wa umma. Tukio hilo liliwaudhi sana wananchi wa Lebanon na kuumiza hisia zao. Mbunge mmoja wa Lebanon alitoa onyo kali kuhusu uhalifu huu wa vyombo vya habari na athari zake kwa umoja wa kitaifa.
-
Palestina lazima ibaki / Watawala wetu wamepotoka kutoka kwenye Misingi ya Umma wa Kiislamu
Mwenyekiti wa Majlisi ya Umoja wa Waislamu wa Pakistan akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuiunga mkono Palestina amesema kuwa, watawala na wanasiasa wa sasa wa nchi hiyo wamejitenga na thamani halisi za Umma wa Kiislamu.
-
Kuuawa Shahidi na Kujeruhiwa kwa Wapalestina 373 ndani ya masaa 24
Wizara ya Afya ya Gaza imetangaza kuuawa Shahidi na kujeruhiwa Wapalestina 373 katika muda wa saa 24 zilizopita na kuongezeka kwa idadi ya Mashahidi wa mauaji ya kimbari na kufikia zaidi ya watu 50,600.
-
Ilitajwa katika Salamu ya Eid al-Fitr:
Kiongozi wa Ansarullah: Watu wa Yemen wanashikamana na kadhia ya Palestina
Akitoa salamu za pongezi za Eid al-Fitr, Sayyid Abdul Malik al-Houthi alisema: "Watu wa Gaza hawakufunga tu Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, bali pia walipata heshima ya Jihadi na Upinzani (Muqawamah) dhidi ya wavamizi."
-
Mashahidi 38 wa Kipalestina; Uovu mpya wa utawala wa Kizayuni huko Gaza
Katika muendelezo wa mashambulizi katika Ukanda wa Ghaza, utawala wa Kizayuni umeua idadi nyingine ya Wapalestina.
-
Takriban Maafisa watano wa ngazi za juu wa Hamas wameuawa Shahidi katika Mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza
Takriban maafisa watano wa ngazi za juu wa Hamas wameuawa katika mashambulizi ya hivi karibuni ya anga ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.
-
Vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza vimeanza tena| Wapalestina 131 wameuawa Shahidi katika mashambulizi ya mabomu ya ndege za Israel
Utawala wa Kizayuni umeshambulia kwa mabomu maeneo mbalimbali ya makazi ya watu katika Ukanda wa Ghaza
-
Mauaji ya raia 2 wa Lebanon kupitia magaidi wa Al-Julani
Magaidi wa Al-Julani wamefanya jinai nyingine katika maeneo ya mpakani mwa Lebanon na Syria.