Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Hujjatul-Islam Muhammad Mahdi Sharif Tabar leo Jumanne, 26 -08- 2025 katika mazungumzo yake, alitangaza kuhusu ushiriki mkubwa wa vikundi vya maombolezo vya Mazandaran kwenye Haram ya Imam Ridha (a.s), na akasema: Mwaka huu kama miaka iliyopita, vikundi vya mkoa huu vimeshiriki kwa hisia na upeo mkubwa katika harakati hii adhimu na kuonesha mapenzi yao kwa Ahlul-Bayt (a.s).
Mkurugenzi huyo wa Tablighat Islami Mazandaran ameongeza kuwa: Ili kuandaa mazingira yanayofaa, kulifanyika mashirikiano na mawasiliano makubwa na taasisi mbalimbali ikiwemo idara za usafirishaji, vyombo vya habari na taasisi za usimamizi. Pia ruhusa maalum zilitolewa kwa ajili ya kuanzishwa kwa vituo vya huduma na mawkib za watu wa Mazandaran huko Mashhad Tukufu.
Akaendelea kusema: Katika safari hii, zaidi ya vikundi 200 vya maombolezo kutoka Mazandaran vilishiriki kwenye hafla mbalimbali na mikusanyiko ya maombolezo mjini Mashhad Tukufu. Moja ya mikusanyiko hiyo ilikuwa mkusanyiko wa pamoja wa vikundi vya Mazandaran katika Sahn Jomhuri, ulioshuhudia wingi wa waombolezaji.
Mkurugenzi huyo alieleza zaidi kuhusu ushiriki wa vikundi vya maombolezo kutoka miji tofauti ya mkoa huo kama vile Behshahr, Sari, Miyanrud, Qaemshahr, Babol, Neka, Babolsar, Amol, Nur, Mahmoudabad na Nowshahr, na akasema: Wote hawa kwa jitihada na mapenzi yao kwa Imam Ridha (a.s) walihudhuria katika harakati hii tukufu. Ibada hii ni miongoni mwa mila ya kihistoria ya watu wa Mazandaran ambapo mwishoni mwa miezi ya maombolezo yao, huonyesha mapenzi yao kwa Imam Ridha (a.s).
Hujjatul-Islam Sharif Tabar akaongeza: Moja ya mambo yenye umuhimu mkubwa mwaka huu lilikuwa ni kukumbuka mashahidi wa Mazandaran waliouawa shahidi wakati wa Vita vya Kulazimishwa. Kwa niaba ya mashahidi hao, majina na kumbukumbu ya mashahidi 49 wa "Uwezo wa Kiislamu" kutoka Mazandaran yaliheshimiwa, na Mazuwwari wa Haram ya Imam Ridha (a.s) waliwakumbuka mashahidi hao wakati wa ziara.
Amesema kuwa: Tunatarajia katika miaka ijayo, vikundi vya maombolezo vya Mazandaran vitashiriki kwa shauku na hamasa zaidi kwenye hafla hizi, na katika njia hii wapate zaidi fursa ya kuhudumia Ahlul-Bayt (a.s) na kufanya ziara ya Imam Ridha (a.s).
Hujjatul-Islam Sharif Tabar amesisitiza: Waombolezaji na mahujaji wasiwasaahau watu wenye matatizo na wagonjwa katika dua zao, na waombe uombezi wa Imam Ridha (a.s) kwa ajili ya kuondoa matatizo yao.
Your Comment