Maafisa wa Hashd al-Shaabi nchini Iraq wameanza kupelekwa rasmi katika njia ya kutoka Najaf kuelekea Karbala kwa ajili ya kulinda usalama wa maelfu ya waumini wanaotembea kwa miguu kwenda kumzuru Imamu Hussein (a.s). Hatua hii ni sehemu ya mpango wa kusimamia matembezi ya mamilioni ya waumini, unaolenga kuimarisha amani, utulivu, na usalama wa mahujaji wa Arbaeen.
Baraza la Mkoa wa Najaf Al-Ashraf limetangaza likizo ya wiki moja kwa ofisi zote za serikali katika mkoa huo, ili kuwezesha ushiriki wa wananchi katika maadhimisho ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s) na kutoa huduma bora kwa maelfu ya mahujaji wanaoelekea Najaf Ashraf.