Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kuna sababu kuu mbili (2) zinazochangia ongezeko la idadi ya Mazuwwari wanaokwenda Kumzuru Mjukuu wa Mtume (saww) huko Karbala.
1. Usalama - Serikali ya Iraq inahakikisha usalama wa mazawwaar, tofauti na Saudi Arabia ambapo mahujaji wengi hukumbana na vitisho na ukosefu wa amani, aidha kutokana na ukandamizaji wa polisi au maafa ya kimkusanyiko.
2. Uhuru wa Kiimani -Nchini Iraq, kila Muumini ana uhuru wa kutekeleza ibada zake kulingana na Dhehebu lake bila bughudha. Hali ni tofauti na Saudi Arabia ambapo Mahujaji wengine huadhibiwa wakituhumiwa kufanya vitendo vya “shirk” kwa mujibu wa mtizamo wao.
Kwa Mantiki hiyo: Ubabe na ukandamizaji wa Saudi Arabia dhidi ya Mahujaji ndio chanzo cha idadi ndogo ya Mahujaji, ilhali ukarimu wa Wananchi wa Iraq, usalama wa Serikali yao, na ukosefu wa ugaidi wa kifikra ndio kichocheo kikuu cha ongezeko la Mazuwwari wa Aba Abdillah Al-Hussein (as), Mjukuu Kipenzi wa Mtume wetu Muhammad (saww).
Your Comment