mahujaji
-
Zaidi ya Mahujaji 5,000 wa Umrah Wamewasili Nchini Saudi Arabia
Shirika la Hija na Ziara nchini Iran limetangaza kuwa idadi ya mahujaji wa Umrah waliopelekwa katika ardhi takatifu tangu kuanza kwa msimu wa Umrah wa mwaka 1445 Hijria (sawa na 1404 kwa kalenda ya Iran), kuanzia tarehe 1 Shahrivar, imefikia zaidi ya watu 5,000.
-
Kwanini Idadi ya Mazuwari Karbala Inaongezeka?:
Ukarimu wa Iraq kwa Mazuwwari na Ukandamizaji wa Saudia kwa Mahujaji: Tofauti ya Idadi ya Mahujaji na Mazuwari
Uhuru wa Kiimani -Nchini Iraq, kila Muumini ana uhuru wa kutekeleza ibada zake kulingana na Dhehebu lake bila bughudha. Hali ni tofauti na Saudi Arabia ambapo Mahujaji wengine huadhibiwa wakituhumiwa kufanya vitendo vya “shirk” kwa mujibu wa mtizamo wao.
-
Waumini wa Kabul Waadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (a.s) Wakihoji Vikwazo vya Safari za Mahujaji (Mazuwwari) wa Afghanistan
Sambamba na kuwadia kwa siku ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s), hafla ya kuadhimisha siku hii ilifanyika katika Kituo cha Fiqhi cha Maasemamu Watakatifu (a.s) upande wa magharibi mwa jiji la Kabul. Washiriki, sambamba na kufanya maombolezo kwa ajili ya Imam Hussein (a.s), walitoa malalamiko makali dhidi ya ukosefu wa uratibu wa kisiasa na kisheria ambao mwaka huu uliwazuia waumini wengi wa Afghanistan kusafiri kwa wingi kwenda Karbala.
-
Wapenzi wa Imam Hussein (as) 36,000 wa Gilan Wajiandikisha kwa ajili ya Arubaini / Waanza Kurudi Nyumbani Taratibu
Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Arubaini mkoa wa Gilan ametangaza kuanza kwa kurejea taratibu kwa mahujaji wa Arubaini mkoani humo na kusema kuwa hadi sasa zaidi ya watu 36,000 kutoka Gilan wamejiandikisha kwenye mfumo wa Samah ili kushiriki katika maadhimisho ya kimataifa ya Arubaini ya Imam Husein (a.s).
-
Saumu ya Arafa | Kwa Mujibu wa Madhehebu ya Shia Ithna Ashari: "Kufunga Siku ya Arafa ni Sunna na si wajibu"
Hoja na Dalili Juu ya Sunna ya Saumu ya Siku ya Arafa: Riwaya kadhaa za Kishia zinaelezea fadhila za kufunga Siku ya Arafa, kama vile riwaya ya Abdur_Rahman bin Abi Abdillah kutoka kwa Abul Hassan (as).