4 Juni 2025 - 14:27
Saumu ya Arafa | Kwa Mujibu wa Madhehebu ya Shia Ithna Ashari: "Kufunga Siku ya Arafa ni Sunna na si wajibu"

Hoja na Dalili Juu ya Sunna ya Saumu ya Siku ya Arafa: Riwaya kadhaa za Kishia zinaelezea fadhila za kufunga Siku ya Arafa, kama vile riwaya ya Abdur_Rahman bin Abi Abdillah kutoka kwa Abul Hassan (as).

Shirika la Habari Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika Madhehebu ya Kishia (Wafuasi wa Ahlul-Bayt a.s), kufunga Siku ya Arafa ni Sunna na si Wajibu. Yaani, kufanya hivyo kuna thawabu, lakini asiyefunga hatakuwa ametenda dhambi.

Ufafanuzi zaidi:

Kufunga Saumu ya Siku ya Arafat na kuwa kwake Sunna:

Kufunga siku ya Arafa ni miongoni mwa matendo ya Sunna yanayopendekezwa kufanywa kwa wale wasiokuwa Mahujaji katika Madhehebu ya Kishia.

Mapendekezo:

Marajii wa kiidini wa Kishia wanapendekeza (wanashauri - wanausia) kufunga Siku ya Arafa kwa wale ambao hawapo katika ibada ya Hijja, na wako kwenye maeneo ya kawaida, huku wakiendelea na ibada na dua mbalimbali.

Masharti:

Iwapo kufunga kutamfanya mtu kuwa dhaifu kiasi cha kushindwa kutekeleza ibada nyinginezo kama vile kusoma dua, ni bora aache kufunga.

Mitazamo tofauti:

Baadhi ya Wanazuoni wa Kishia wanatambua kufunga Siku ya Arafa kwa Mahujaji kuwa ni Jambo lisiloruhusiwa kwao, kwa kuwa Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) hakuwa akifunga Saumu ya Siku ya Arafa alipokuwa katika Uwanja wa Arafa.

Hoja na Dalili Juu ya Sunna ya Saumu ya Siku ya Arafa:

Riwaya kadhaa za Kishia zinaelezea fadhila za kufunga Siku ya Arafa, kama vile riwaya ya Abdur_Rahman bin Abi Abdillah kutoka kwa Abul Hassan (a.s.) inayosema: 

"Kufunga Siku ya Arafa ni sawa na kufunga mwaka mzima".

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha