Hijjah
-
Rais Pezeshkian: Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi kwa Mahujaji Uliweka Alama Muhimu katika Hija ya Mwaka Huu
Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji wa Kiislamu umeifanya Hijja ya mwaka huu kuwa ya kipekee, huku akiwapongeza viongozi na watendaji wa Hijja kwa kuhakikisha mahujaji wa Iran wanatekeleza ibada zao kwa usalama, afya njema na heshima.
-
Zaidi ya Huduma 164,000 za Matibabu Zatolewa kwa Mahujaji wa Iran katika Ardhi Takatifu
Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Iran imetangaza kuwa imewapatia mahujaji wa Iran zaidi ya huduma 164,000 za afya na matibabu wakati wa msimu wa Hija, huku mahujaji tisa wakiripotiwa kulazwa hospitalini na wanne kufariki dunia hadi sasa.
-
Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum Atoa Nasaha za Eid al-Adha na Hijja: Ibada Ifanywe kwa Ikhlasi na Si Kujionesha Mitandaoni
Sheikh Profesa Alhad Mussa Salum amesisitiza umuhimu wa uelewa sahihi wa ibada za Eid al-Adha na Hijja. Ameeleza kuwa kondoo ni mnyama bora zaidi kwa kuchinjwa katika Eid al-Adha endapo anapatikana, na hata nyama yake ni bora zaidi Bali Kondoo Ndiye asili ya ibada hiyo. Kuhusu Hijja, amebainisha kuwa ni ibada ya kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu kupitia Nabii Ibrahim (as), na huleta utakaso wa dhambi kwa mja. Ameonya baadhi ya mahujaji kukosa maandalizi ya kiroho na kurejea katika dhambi baada ya Hijja. Ameikosoa tabia ya kutumia ibada ya Hijja kwa kujionesha mitandaoni kupitia Picha za “selfie”, akisisitiza kuwa ibada ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee. Amemalizia kwa kusisitiza msingi wa ikhlasi na kuepuka riyaa katika ibada zote.
-
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu:
“Silaha ya Allahu Akbar” italeta uamsho wa Umma wa Kiislamu"
Katika ujumbe wake kwa mnasaba wa msimu wa Hijja ya mwaka 1447 Hijria, Ayatollah Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei amesisitiza kuwa kauli ya “Allahu Akbar” imekuwa silaha ya msingi ya Umma wa Kiislamu katika kupambana na dhulma na ubeberu. Ameeleza kuwa uamsho wa Kiislamu utaendelea kuenea duniani kupitia mshikamano wa Waislamu, huku akisisitiza umuhimu wa kujitenga na Marekani pamoja na utawala wa Kizayuni katika nyanja za kisiasa na kijamii.