26 Oktoba 2025 - 18:34
Rais wa Kituo cha Huduma za Vyuo vya Dini Atoa Wito wa Kuwezesha Uwepo wa Wanafunzi na Mazuwwari wa Kiiran Katika Maeneo Matukufu ya Iraq

Katika kikao rasmi kilichofanyika kati ya Hujjatul-Islam wal-Muslimin Dkt. Mir Muhammadi, Rais wa Kituo cha Huduma za Vyuo vya Dini (Hawza), na Dkt. Al-Sadiq, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Iraq, pande zote mbili zilikubaliana juu ya umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kitamaduni na kidini pamoja na kufanikisha uwepo wa wanafunzi wa dini na mahujaji wa Kiirani katika maeneo matukufu ya Iraq (Atabat Aaliyat).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-, Dkt. Mir Muhammadi alisisitiza katika kikao hicho umuhimu wa kuboresha huduma za kidini na kiutamaduni, na akatoa wito kwa ubalozi wa Iran nchini Iraq kushirikiana kwa karibu katika kuwaunga mkono wanafunzi wa dini na Mazuwwari wa Kiirani.

Akiwasilisha ripoti kamili kuhusu shughuli za kituo chake, Dkt. Mir Muhammadi alieleza kuwa urahisishaji wa safari na uwepo wa wanafunzi wa dini na mahujaji katika maeneo matukufu ni moja ya malengo makuu ya kituo hicho.

Aidha, alibainisha kuwa ziara za wanafunzi na Mazuwwari wa Kiiran katika maeneo matukufu hazina tu thamani ya kiroho, bali pia zinachangia pakubwa katika kueneza utamaduni wa Kiislamu na kuimarisha uhusiano wa kielimu kati ya vyuo vya dini vya Iran na Iraq. Alisisitiza kuwa kuweka mazingira bora zaidi kutawanufaisha zaidi makundi hayo mawili.

Katika maelezo yake zaidi, Dkt. Mir Muhammadi alieleza kuwa hatua mbalimbali za kuwasaidia wanafunzi wa dini walioko Najaf zimekuwa zikitekelezwa kwa mujibu wa maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi na kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Al-Mustafa na uongozi wa Hawza ya Kiume.

Uhusiano chanya kati ya Hawza ya Najaf na Hawza ya Qom

Kwa upande wake, Balozi wa Iran nchini Iraq, Dkt. Al-Sadiq, alitoa taarifa kuhusu hali ya kisiasa na kijamii ya Iraq na akasisitiza umuhimu wa mikutano ya mara kwa mara na Mwakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Dini nchini Iraq, Ayatollah Sayyid Hosseini, ili kuimarisha ushirikiano na kushughulikia masuala yanayowahusu Wairani na wanafunzi wa dini.

Alitaja pia ziara ya hivi karibuni ya Ayatollah al-Udhma Jawadi Amoli nchini Iraq na mapokezi makubwa kutoka kwa wanazuoni na wanafunzi wa Najaf, akisema kuwa:

“Alhamdulillah, uhusiano kati ya Hawza ya Najaf na Hawza ya Qom ni mzuri na wa kimaendeleo. Lazima juhudi ziendelee ili kuimarisha zaidi uhusiano wa kielimu na kiroho kati ya pande hizi mbili.”

Balozi Al-Sadiq pia alizungumzia baadhi ya hatua zilizochukuliwa na ubalozi kuhusu masuala ya ukaaji, afya na taratibu za kiutawala za wanafunzi wa dini wa Kiirani wanaoishi Iraq, akibainisha kuwa masuala hayo yanapewa umuhimu na msaada kamili kutoka ubalozi wa Iran.

Mwisho wa kikao, Balozi Al-Sadiq alikaribisha mapendekezo yaliyowasilishwa na Kituo cha Huduma za Vyuo vya Dini, na akaonyesha utayari wake wa kushirikiana kikamilifu katika kurahisisha safari na uwepo wa wanafunzi wa dini na mahujaji wa Kiirani katika maeneo matukufu ya Iraq.

Kikao hiki kilifanyika katika muktadha wa kuimarisha uhusiano kati ya taasisi za kielimu za kidini (Hawza) na taasisi za kidiplomasia za Iran nje ya nchi, kwa lengo la kupanua ushiriki wa wanafunzi wa dini na mahujaji katika maeneo matukufu ya Iraq kama vile Najaf, Karbala, Kadhimayn na Samarra.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha