Ziara
-
Msemaji wa Mahakama ya Iran: Ziara ya Ejei Nchini India Ilikuwa na Mikutano Mingi na ya Kiwango cha Juu
Ziara ya Mkuu wa Mahakama ya Iran, Hujjatul-Islam Gholam-Hossein Mohseni Ejei, nchini India kwa ajili ya mkutano wa wakuu wa mahakama za nchi wanachama wa BRICS ilihusisha mikutano mbalimbali na viongozi wa mahakama, viongozi wa dini, wafanyabiashara pamoja na wawakilishi wa jamii tofauti za kidini.
-
Tabatabai: Ziara ya Mkuu wa Jeshi la Pakistan Nchini Iran Ilikuwa na Matokeo Makubwa ya Kidiplomasia
Msaidizi wa Rais wa Iran katika masuala ya mahusiano ya umma, Mehdi Tabatabai, amesema ziara ya Mkuu wa Jeshi la Pakistan, Field Marshal Asim Munir, nchini Iran ilikuwa na matokeo muhimu sana ya kidiplomasia, akikanusha baadhi ya makadirio ya vyombo vya habari kuhusu ziara hiyo.
-
Zaidi ya Watu Milioni Mbili Wamtembelea Imam Shahidi kwa Niaba Yake Katika Ziara ya Arbaeen
Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Masuala ya Hija na Ziara, Hujjatul-Islam Sayyid Abdulfattah Nawab, amesema zaidi ya mahujaji milioni mbili walifanya ziara ya Arbaeen kwa niaba ya Imam Shahidi mwaka huu. Pia amesimulia ushauri wa Imam Shahidi kwamba ibada ya Hija ya Sunnah isifanywe kwa niaba yake pekee, bali waumini wengine washirikishwe katika thawabu yake.
-
Arubaini ya Imam Hussein Yafanyika Seoul; Sauti ya “Ya Hussein” Yasikika Moyoni mwa Korea Kusini
Kwa kusoma Ziyarat ya Arubaini na kuomboleza kwa ajili ya Imam Hussein (as), Mashia na wapenzi wa Ahlul-Bayt (as) mjini Seoul wamehuisha kumbukumbu ya Karbala na kusisitiza kaulimbiu: “Mapenzi ya Hussein yanatuunganisha.”
-
Pakistan: Ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani Tehran Kulenga Kuimarisha Amani na Usalama wa Kikanda
Pakistan imesema ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Mohsin Naqvi, nchini Iran inalenga kuendeleza mashauriano na Tehran kuhusu kuimarisha uhusiano wa pande mbili, ushirikiano wa kiusalama na juhudi za kuimarisha amani na utulivu katika eneo.
-
Iran na Iraq Zakubaliana Kuimarisha Ushirikiano wa Kisayansi na Vyuo Vikuu
Ziara ya Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Iran nchini Iraq imefungua njia mpya ya kuimarisha ushirikiano katika sekta za sayansi, teknolojia na elimu ya juu kupitia mazungumzo na viongozi wakuu wa Iraq.
-
Mashambulizi ya Saudi Arabia na Marekani dhidi ya Hashd al-Shaabi Yazua Maswali Kufuatia Ziara ya Waziri Mkuu wa Iraq Marekani
Mashambulizi yaliyotekelezwa na Saudi Arabia na Marekani dhidi ya vituo vya Hashd al-Shaabi yamesababisha vifo vya zaidi ya wanajeshi 20 wa Iraq, huku yakizua mjadala kuhusu matokeo ya ziara ya Waziri Mkuu mpya wa Iraq nchini Marekani na mkutano wake na Rais wa Marekani, Donald Trump.
-
Zaidi ya wageni 434,000 wapita katika vituo vya mipakani Khuzestan kuelekea ziara ya Arbaeen
Zaidi ya wageni 434,000, wakiwemo Wairani na raia wa kigeni, wamevuka kupitia vituo vya mipakani vya Shalamcheh na Chazabeh katika Mkoa wa Khuzestan, kusini-magharibi mwa Iran, kwa ajili ya kushiriki katika ziara ya Arbaeen ya Imam Hussein (as).
-
Msemaji wa Serikali ya Iran: Mkakati Wetu Unategemea Uwezo wa Ndani na Uungwaji Mkono wa Wananchi
Msemaji wa Serikali ya Iran, Fatemeh Mohajerani, amesema kuwa Mkakati wa Serikali unategemea Uwezo wa Ndani na Uungwaji Mkono wa Wananchi, akisisitiza kuwa Umoja wa Kitaifa wa Wananchi wa Iran utaiwezesha Nchi hiyo kupata Ushindi dhidi ya Maadui wanaolenga Maisha ya Watu, Shule na Hospitali.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Atembelea na Kutoa Heshima Katika Maqamu Takatifu za Imam Hussein (AS) na Hazrat Abolfazl Abbas (AS) nchini Iraq
Waziri wa Mambo ya Nje wa Abbas Araghchi amefanya ziara katika mji mtakatifu wa Karbala, ambapo alitembelea maqamu takatifu za Imam Hussein ibn Ali na Al-Abbas ibn Ali na kutoa heshima zake wakati wa ziara yake rasmi nchini Iraq.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi Akutana na Mwenzake wa Iraq Jijini Baghdad
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Seyyed Abbas Araghchi, amewasili Baghdad kwa ziara rasmi na kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq, Fouad Hussein, kwa lengo la kujadili masuala ya pande mbili na maendeleo ya kikanda.
-
Pakistan: Ziara ya Rais Pezeshkian Islamabad Yaakisi Dhamira ya Pamoja ya Amani na Maendeleo ya Kikanda
Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan imesema ziara rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, nchini Pakistan inaonesha azma ya pamoja ya Tehran na Islamabad ya kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kitamaduni, pamoja na kuendeleza amani, utulivu na maendeleo endelevu katika eneo.
-
Rais Pezeshkian: Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi kwa Mahujaji Uliweka Alama Muhimu katika Hija ya Mwaka Huu
Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji wa Kiislamu umeifanya Hijja ya mwaka huu kuwa ya kipekee, huku akiwapongeza viongozi na watendaji wa Hijja kwa kuhakikisha mahujaji wa Iran wanatekeleza ibada zao kwa usalama, afya njema na heshima.
-
Njama ya Aibu: Upinzani wa India walaani ziara ya Modi nchini Israel
Ziara ya siku ya Jumatano ya Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India, kwenda Israel, imezua ukosoaji mkubwa kutoka kwa vyama na makundi ya mrengo wa kushoto nchini humo. Makundi hayo yamemshutumu kiongozi huyo wa kitaifa mwenye msimamo wa Uhindu kwa kushirikiana au kuunga mkono vita vinavyoendelea vya Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza. Wakosoaji wanasema kuwa ziara hiyo inapingana na msimamo wa kihistoria wa India wa kuunga mkono haki za Wapalestina na suluhisho la mataifa mawili, na wameitaka serikali kutoa maelezo ya wazi kuhusu madhumuni ya safari hiyo pamoja na makubaliano yaliyofikiwa.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Akutana na Naibu Mkuu wa Baraza Kuu la Kishia Lebanon Beirut
Wakati wa ziara yake rasmi mjini Beirut, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Seyyed Abbas Araghchi, alikutana na Sheikh Ali Al-Khatib, Naibu Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia nchini Lebanon. Mazungumzo yao yalijikita katika maendeleo ya kikanda, umuhimu wa umoja wa Kiislamu, na kuimarisha ushirikiano wa kidini na kisiasa kwa ajili ya uthabiti na mshikamano wa Lebanon.
-
Heshima na Unyenyekevu wa Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kwa Wazee | Sala ya Ijumaa - Masjid Abdallah Rashid - Zanzibar
Rais Dkt. Mwinyi pia ameswali Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa 'Abdallah Rashid', ikiwa ni hatua inayotekeleza utaratibu wake wa kawaida wa kusali katika Misikiti mbalimbali nchini, kwa lengo la kuimarisha mshikamano wa kijamii na kudumisha mahusiano ya karibu kati ya Viongozi na Waumini.
-
Mkuu wa Jeshi la Iran Amir Hatami Akikagua Ngome za Kijeshi za Mipakani pamoja na Brigedi za Jeshi la Ardhini
Ziara hii inakuja wakati Iran inasisitiza kuimarisha usalama wa mipaka yake na kuonyesha utayari wa jeshi katika kukabiliana na changamoto za kijeshi bila kukosa tahadhari ya kisiasa, hasa kutokana na mvutano uliopo katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Al-Mustafa na Chuo Kikuu cha Félix Houphouët-Boigny katika Njia ya Kuimarisha Ushirikiano wa Kitaaluma
Mkutano huu unaakisi nia ya dhati ya pamoja ya vyuo hivyo viwili katika kuinua ubora wa elimu ya juu, kupanua ushirikiano wa baina ya vyuo vikuu, na kubadilishana uzoefu wa kielimu nchini Côte d’Ivoire.
-
Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Atoa Maagizo Mazito: Wajawazito Kuhudumiwa Kwa Haraka na Dawa Kupatikana Hospitalini
Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi kupitia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya: a) Vifaa tiba, b) Dawa, c) Na maboresho ya miundombinu ya afya.
-
Qalibaf: Pakistan ni rafiki wa kweli katika nyakati zote
Spika wa Bunge la Iran ameandika kwenye ukurasa wake binafsi katika mitandao ya kijamii kuwa:“Kwa mwaliko maalumu wa Mheshimiwa Spika wa Bunge la Kitaifa la Pakistan, nimeelekea nchini humo. Kuimarisha uhusiano wa pande mbili kati ya mataifa haya mawili ndugu - hususan katika nyanja za ushirikiano wa kiuchumi na kiusalama - kutakuwa ndiyo mhimili mkuu wa ziara hii.”
-
Rais wa Kituo cha Huduma za Vyuo vya Dini Atoa Wito wa Kuwezesha Uwepo wa Wanafunzi na Mazuwwari wa Kiiran Katika Maeneo Matukufu ya Iraq
Katika kikao rasmi kilichofanyika kati ya Hujjatul-Islam wal-Muslimin Dkt. Mir Muhammadi, Rais wa Kituo cha Huduma za Vyuo vya Dini (Hawza), na Dkt. Al-Sadiq, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Iraq, pande zote mbili zilikubaliana juu ya umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kitamaduni na kidini pamoja na kufanikisha uwepo wa wanafunzi wa dini na mahujaji wa Kiirani katika maeneo matukufu ya Iraq (Atabat Aaliyat).
-
Sheikh Hemed Jalala na Sheikh wa Mkoa wa Tabora (BAKWATA) waonyesha: Matendo ya Hekima Yanayounganisha Watu na Kuimarisha Umoja wa Kiislamu
Kwa hakika, ziara hii ni kielelezo cha Uislamu wa kweli uliofundishwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w.) - Uislamu wa upendo, udugu, na umoja. Kama alivyonena Imam Ali (a.s.): "Kuweni walinganizi wa watu bila kutumia maneno yenu, bali kwa matendo yenu.” (Nahjul-Balagha, Hikma 31)
-
Maulana Sheikh Hemed Jalala Aendelea kuimarisha Umoja wa Waislamu Kupitia Ziara ya Kidini Nchini Tanzania
Katika moja ya sehemu za ziara yake, Maulana Sheikh Hemed Jalala alitembelea Mkoa wa Kigoma, ambapo alipokelewa kwa mapokezi mazuri kutoka kwa waumini na viongozi wa dini wa eneo hilo. Moja ya matukio muhimu katika ziara hiyo ni kukutana kwake na Sheikh wa Mkoa wa Kigoma (BAKWATA), Samahat Sheikh Hassan Kiburwa, katika ofisi za BAKWATA Mkoa wa Kigoma, ambapo viongozi hao wawili walifanya mazungumzo ya kina kuhusu maendeleo ya Uislamu, umoja wa Waislamu, na namna bora ya kuimarisha harakati za kidini nchini.