Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AhlulBayt (a.s)–ABNA– Gavana wa Karbala, Nasiif Jasim Al-Khutabi, leo (Jumapili) ameeleza kwamba operesheni ya kigaidi dhidi ya moja ya Husseiniyya zilizoko njiani mwa mahujaji wa kuelekea Karbala imefanikishwa kuzuiwa.
Al-Khutabi amebainisha kwamba wanachama 22 wa kundi la kigaidi waliokuwa wakipanga mashambulio ya kigaidi na kushambulia washiriki wa matembezi ya Arubaini, wamebainika na kukamatwa.
Kwa mujibu wake, magaidi hao walipanga kuweka vilipuzi njiani na kuvilipua ili kulenga maafisa wa usalama na mahema ya maombolezo ya Husseiniyya yaliyoko katika njia ya mahujaji, hususan katika njia ya kusini.
Gavana huyo amesema kuwa magaidi hao walihusiana na kundi la Daesh (ISIS) na walikuwa na mawasiliano na baadhi ya pande za nje ya Iraq, zikiwemo baadhi zilizo na uhusiano na utawala wa Kizayuni (Israel).
Your Comment