Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) —ABNA— Ali al-Badri, Mkuu wa Idara ya Habari ya Haramu ya Abbas, katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Al-Mirbad alisema:
“Utabiri unaonyesha kuwa idadi ya mahujaji mwaka huu itazidi ile ya mwaka jana; mwaka jana idadi ya mahujaji ilizidi milioni 21.”
Ameongeza kuwa maandalizi yote yamekamilishwa mapema, na Haramu ya Abbas imepanga shughuli zake kwa kuzingatia takwimu za miaka iliyopita ili kutoa huduma bora zaidi, ikiwemo kuratibu harakati za mahujaji, kutoa huduma za kupunguza athari ya joto kali, na kutumia rasilimali zote ilizonazo.
Al-Badri pia amewasisitiza mahujaji wa Arbaeen kushirikiana na vyombo vya usalama, wenzao, mawakibu za Husseiniyya na taasisi zote za huduma ili kuhakikisha maadhimisho ya ziara ya Arbaeen yanafanyika kwa njia bora na yenye heshima kubwa.
Your Comment