Mwakilishi mwenye mamlaka kamili wa Ayatollah Sistani nchini Iran amesema kuwa Arbaeen ni fursa kubwa sana kwa wasimamizi na wenye dhamana wa tukio hili la kimataifa, na hawapaswi kupuuzia au kughafilika na thawabu na malipo makubwa yanayopatikana kutokana nalo.
Serikali ya Punjab imewaita wamiliki wa vibali vya kufanya maombolezo, waandaaji wa vituo vya kutoa huduma za bure (maisha ya Sadaka) na wajumbe wa kamati za ulinzi, na kuwashinikiza watangaze rasmi kujitenga na matembezi ya Arbaeen kuelekea Karbala.
Haramu Takatifu ya Abbas imebashiri kuwa idadi ya mahujaji watakaoingia katika mkoa wa Karbala kwa ajili ya maadhimisho ya Arbaeen mwaka huu itaongezeka ikilinganishwa na mwaka uliopita.