Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Maulana Sheikh Hemed Jalala, na ambaye ni Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna Ashari Tanzania (TIC), amefanya ziara ya kumjulia hali mwanachuoni mahiri wa Kiislamu, Sheikh Bakari Mbelango, ambaye kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mloganzila baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ampe afueni ya haraka na amuwekee wepesi katika kila jambo. Uwepo wake ni hazina kwa Uislamu na Waislamu.
Your Comment