Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum anafafanua kuwa swaumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhan si adhabu, bali ni ibada iliyojaa huruma ya Mwenyezi Mungu. Kufunga kunalenga kutuponya kiroho na kimwili, kuimarisha nafsi, na kutufundisha subira, kama ambavyo Daktari (Tabibu) humlazimisha mgonjwa kunywa dawa chungu, lakini sio kwa lengo la kumuadhibu, bali ili apone. Swaumu ni fursa ya kujenga uhusiano thabiti baina ya Mja na Mola wake (swt) na kupata manufaa mapana katika maisha yetu.