Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Uongozi Mkuu wa Haram Tukufu ya Askariyayn umempokea kwa heshima kubwa Kiongozi wa Dini, Marjaa wa Kiislamu Ayatollah Sheikh Abdullah Jawadi Al-A'muli, baada ya kupata fursa ya kutembelea Makaburi Matukufu ya Maimamu wawili wa Ahlulbayt (as), Imam Al-Askari na Imam Al-Hadi (amani iwe juu yao) pamoja na sehemu tukufu ya Sardab, iliyopo katika mji wa Samarra.
Katika heshima ya ziara hii tukufu, Haram ilifanya hafla maalum ya kumuenzi Sheikh Jawadi Al-A'muli, sambamba na kuzinduliwa kwa kitabu chake kipya chenye kichwa:
Sharh Ziyarat Al-Jami'a Al-Kabira (Ufafanuzi wa Ziara ya Jami'a Kubwa), riwaya ya Imam Al-Hadi (amani iwe juu yake).
Wakati wa hafla hiyo, zawadi zenye baraka zilitolewa kwa Ayatollah Sheikh Jawadi A'muli, ikiwemo bendera ya Maqam wa Ma-Imamu Wawili Askariyayn, kama ishara ya kutambua juhudi zake kubwa katika elimu ya Dini.
Kwa upande wake, Sheikh Al-Amuli aliikabidhi Haram nakala ya kitabu chake kipya kwa ajili ya matumizi ya watafiti katika Mji Mtukufu wa Samarra.
Your Comment