Mtume Mtukufu (s.a.w.w) katika ubora na thawabu ya kumswalia Bibi Fatimah Zahra (a.s) amesema: “Ewe Fatimah! Yeyote atakayekuswalia na kukutumia salamu, Mwenyezi Mungu atamsamehe na popote nitakapokuwa katika Pepo atamuunganisha nami.”
Katika heshima ya ziara hii tukufu, Haram ilifanya hafla maalum ya kumuenzi Sheikh Jawadi Al-A'muli, sambamba na kuzinduliwa kwa kitabu chake kipya chenye kichwa: Sharh Ziyarat Al-Jami'a Al-Kabira