haram tukufu
-
Ayatollah Sheikh Jawadi Amuli Atembelea Makao ya Maimamu wa Ahlul-Bayt (as) Samarra, Akaribishwa kwa Heshima Kubwa
Katika heshima ya ziara hii tukufu, Haram ilifanya hafla maalum ya kumuenzi Sheikh Jawadi Al-A'muli, sambamba na kuzinduliwa kwa kitabu chake kipya chenye kichwa: Sharh Ziyarat Al-Jami'a Al-Kabira
-
Waqfu wa Kiongozi wa Mapinduzi 5 / Mtoaji mkubwa wa Waqfu wa Nakala za Maandishi ya Kale katika historia ya Haram Tukufu ya Razavi
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, pamoja na Waqfu mbalimbali alizotoa kwa Haram Tukufu ya Razavi katika zaidi ya miaka 40 iliyopita, ametoa waqfu wa vitabu vingi vya kale kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Haram Tukufu ya Razavi.
-
Imam Ali (a.s) Katika Kurasa za Historia:
Elimu na Maarifa, Ibada na Ucha Mungu, Ujasiri na Ushujaa, na Upole na Huruma ya Imam Ali (a.s)
Imam Ali (a.s) alipigwa upanga na mtu aliyejulikana kwa jina la Abdur Rahman bin Muljim Muradi (laana iwe juu yake milele). Imam Ali (a.s) alikufa Shahidi siku tatu baadaye katika usiku wa 21 wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Imam Ali bin Abi Talib (a.s) ni shakhsia wa pili mkubwa katika Uislamu baada ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), na anaelezwa katika historia ya Uislamu kuwa alikuwa jasiri na shujaa wa kupigiwa mfano, mwenye imani thabiti, mwenye akhlaki njema, mwenye elimu na uadilifu usio na kifani.