Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq, siku ya Alhamisi, ilieleza kuwa Iraq imewapokea mahujaji wa kigeni wapatao milioni 4.1 kutoka kwenye misafara mbalimbali ya kimataifa waliokuja kushiriki katika Ziara ya Arubaini.
Taarifa ya wizara hiyo ilisema kuwa idadi hiyo ya mahujaji inatoka katika mataifa 140 tofauti duniani.
Awali, Mkuu wa Kitengo cha Habari za Usalama cha Iraq alisisitiza kuwa hadi sasa hakujakuwa na tishio lolote la kiusalama katika shughuli hii ya ziara.
Kadhalika, Gavana wa Mkoa wa Karbala alibainisha kuwa idadi ya mahujaji mwaka huu imeongezeka ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Your Comment