Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Samahat Sheikh Kadhim Abbas, Mudir wa Hawza za Bilal Muslim Tanga, Tanzania, leo hii Alhamisi Machi 10, 2025 amefanya ziara katika Hawza ya Imam Ali (a.s) Pangani. Lengo la ziara hii ni kufuatilia na kutekeleza hatua muhimu za uboreshaji wa Sekta ya elimu katika Hawza za Bilal Muslim Tanga.
Samahat Sheikh Kadhim, katika ziara hii, amefanikiwa kukutana na Walimu wa Hawzat Imam Ali (a.s) pamoja na Wanafunzi. Na katika hotuba yake kwa Wanafunzi wa Hawza hii, ameshiria juu ya umuhimu wa kuzingatia masomo yao na kusoma kwa bidii ili kuhakikisha wanayafikia malengo matukufu ya kuchuma maarifa ya Dini Tukufu ya Kiislamu. Aidha, aliwanukulia baadhi ya maneno mazuri yenye hekima kutoka kwa Imam Ali (a.s), na kuwapa nasaha mbali mbali zenye mafungamano na uchumaji wa elimu na maarifa ya Kiislamu.
Katika kuthamini, kushukuru na na kuheshimu sapoti inayotolewa katika uwanja huu wa Hawza ya Kielimu, Kitengo cha Ripoti za Hawza Bilal Muslim Pangani, kimetoa pongezi za dhati kwa Taasisi ya Bilal Muslim Tanga Branch, kwa kuendelea kuimarisha sekta ya Ki_Hawza na Tabligh kwa ujumla.
Your Comment