Wito
-
Mufti wa Tanzania Atoa Wito wa Kulinda Amani na Kuepuka Uchochezi wa Kidini na Maandamano Yanayopangwa Kufanyika 9 Disemba
"Tuepuke upepo mbaya unaosambazwa kwa chuki za kidini. Sisi Waislamu hatukatazwi kuishi kwa wema na wasiokuwa Waislamu. Maisha ya watu lazima yalindwe,” alisema Mufti.
-
JMAT Yatoa Wito wa Maridhiano na Amani, Funga ya Siku Tatu na Maombi ya Kitaifa kwa ajili ya Umoja wa Kitaifa
Mwenyekiti wa JMAT, Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum, amesema: "Matukio ya baada ya Uchaguzi yameacha majeraha ya kisaikolojia na kuchochea hisia za kidini, hivyo kunahitajika hatua za haraka kuimarisha umoja wa kitaifa. Amehimiza maombi hayo yashirikishe waumini wa madhehebu zote na kufanyika kwa mfumo mmoja na Kwa siku moja kitaifa".
-
Kuendelea kwa Mjadala Mkali Kuhusu Mbio ya Hisani ya Msikiti wa East London; Wito Watolewa kwa Mapitio ya Sera ya Utenganisho wa Jinsia
Baada ya mashambulizi makubwa ya vyombo vya habari vya Uingereza dhidi ya mbio ya hisani iliyoandaliwa na Msikiti wa East London kwa sababu ya utenganishaji wa kijinsia, Tume ya Usawa na Haki za Kibinadamu ya Uingereza imeitangaza kwamba waandaaji wa tukio hilo wamekubali kupitia upya sera zake kabla ya awamu ijayo ya mashindano. Hata hivyo, msikiti huo umeeleza kwamba matukio kama hayo yapo kwa wingi katika maeneo mbalimbali ya Uingereza-ikiwemo mashindano maalumu ya wanawake na vipindi vya kuogelea vinavyoandaliwa katika vituo vya jamii ya Kiyahudi-lakini hakuna hata moja kati ya matukio hayo yaliyowahi kusababisha mjadala au msukosuko kama huu.
-
Rais wa Lebanon: Atoa Wito wa kupata msaada kutoka Benki ya Dunia
"Tumejitolea kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano, lakini utawala wa Kizayuni unaendelea kuvunja makubaliano hayo"
Rais wa Lebanon, katika kikao chake na ujumbe wa Benki ya Dunia, alisisitiza kujitolea kwa nchi yake kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano, huku akilaani kuongezeka kwa uvamizi unaofanywa na utawala wa Kizayuni katika eneo la kusini mwa Lebanon. Aidha, aliomba taasisi za kifedha za kimataifa zitoe msaada kwa mchakato wa maendeleo na mageuzi nchini Lebanon.
-
Waziri Mkuu wa Lebanon: Israel lazima iondoke kwenye ardhi yetu
Wito wa kuimarisha jeshi la Lebanon: Waziri Mkuu Salam aliendelea kusisitiza kuwa: “Utekelezaji wa sera ya serikali ya kuhakikisha silaha zinakuwa mikononi mwa dola pekee — iwe kusini au kaskazini mwa Mto Litani — unategemea kuharakishwa kwa misaada ya kijeshi kwa jeshi la Lebanon na vikosi vya usalama wa ndani.”
-
Rais wa Kituo cha Huduma za Vyuo vya Dini Atoa Wito wa Kuwezesha Uwepo wa Wanafunzi na Mazuwwari wa Kiiran Katika Maeneo Matukufu ya Iraq
Katika kikao rasmi kilichofanyika kati ya Hujjatul-Islam wal-Muslimin Dkt. Mir Muhammadi, Rais wa Kituo cha Huduma za Vyuo vya Dini (Hawza), na Dkt. Al-Sadiq, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Iraq, pande zote mbili zilikubaliana juu ya umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kitamaduni na kidini pamoja na kufanikisha uwepo wa wanafunzi wa dini na mahujaji wa Kiirani katika maeneo matukufu ya Iraq (Atabat Aaliyat).
-
Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi:
“Vikosi vya Ulinzi vya Iran vimewapiga maadui zao Kofi lisilosahaulika”
Jenerali Mousavi alisema kuwa kipindi cha masomo ya kijeshi kwa wanafunzi hao kilitokea katika wakati wa kipekee - wakati ambao muqawama ulithibitisha ushindi wa imani juu ya dhulma na ubabe wa kimataifa.
-
Ombi la Kikosi cha Uthabiti na Uimara cha Muqawama kwa Serikali za Dunia: “Tuunge Mkono”
Waandaji wa Kikosi cha Uthabiti na Uimara cha Muqawama wametoa wito kwa Serikali za Dunia kusaidia harakati za meli za kikosi hiki kuelekea Ukanda wa Gaza.
-
Taarifa ya Hizbullah na Harakati ya Amal zinatoa wito wa mkusanyiko wa kuonyesha upinzani dhidi ya maamuzi ya serikali
Katika taarifa ya Hizbullah na Harakati ya Amal ilisemwa: 'Enyi wafanyakazi na wazalishaji wa Lebanon, tumekuwa wavumilivu kwa muda mrefu juu ya changamoto zinazolikumba taifa letu, na sasa umefika wakati wa kuonyesha msimamo wetu wa kitaifa kwa pamoja.' Wakaongeza: 'Tuna miadi ya kusimama kwa pamoja kama taifa, kuonyesha kupinga kwetu njia ya kujisalimisha na kutii bila masharti, na kulinda nguvu na uhuru wa Lebanon'.
-
Leo tuko katika vita kamili -vya jumla- kati ya Imani na Ukafiri |Wito wa uhamasishaji wa Vyombo vya Habari na Ubainishaji Mzuri ili Kutetea Mapinduzi
Leo hii, ndio maana tunaona kila mtu ulimwenguni akifurahi kwamba Israeli inapigwa na Makombora ya Iran. Pia tunaona umoja wa kitaifa ndani ya nchi, ambapo kila mtu analaani hujuma za utawala wa Kizayuni dhidi ya nchi yetu, isipokuwa watu wachache wabaya na waliolaaniwa ambao hata majina yao hayaruhusiwi kutamkwa na kutajwa.
-
Wito wa Kwanza | Tamasha la Kitaifa la Ushairi wa Ghadir Kufanyika Katika Chuo Cha Jamiat Al-Mustafa Foundation - Mbezi Beach - Dar-es- Salaam
Washairi wa Kiislamu kutoka sehemu mbalimbali watahudhuria kwa ajili ya kusoma mashairi yanayogusa nyoyo kuhusu: Tukio la Ghadir, Mapenzi kwa Ahlul-Bayt(as), na mafundisho ya Kiislamu.