17 Juni 2025 - 17:11
Leo tuko katika vita kamili -vya jumla- kati ya Imani na Ukafiri |Wito wa uhamasishaji wa Vyombo vya Habari na Ubainishaji Mzuri ili Kutetea Mapinduzi

Leo hii, ndio maana tunaona kila mtu ulimwenguni akifurahi kwamba Israeli inapigwa na Makombora ya Iran. Pia tunaona umoja wa kitaifa ndani ya nchi, ambapo kila mtu analaani hujuma za utawala wa Kizayuni dhidi ya nchi yetu, isipokuwa watu wachache wabaya na waliolaaniwa ambao hata majina yao hayaruhusiwi kutamkwa na kutajwa.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Ayatullah Ramezani aliuchukulia utawala wa Kizayuni kuwa ndio serikali mbovu zaidi katika historia kuhusiana na ukiukaji wa haki za binadamu na akasema: "Katika historia ya Mwanadamu hakuna serikali iliyokiuka haki za binadamu kama utawala haram wa Kizayuni. Kuna visa vingi vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa mujibu wa matamshi na maazimio ya Umoja wa Mataifa."

Leo hii, ndio maana tunaona kila mtu ulimwenguni akifurahi kwamba Israeli inapigwa na Makombora ya Iran. Pia tunaona umoja wa kitaifa ndani ya nchi, ambapo kila mtu analaani hujuma za utawala wa Kizayuni dhidi ya nchi yetu, isipokuwa watu wachache wabaya na waliolaaniwa ambao hata majina yao hayaruhusiwi kutamkwa na kutajwa.

Kila mtu aliye na damu ya Iran ndani ya Iran amelaani uchokozi huu. Hukmu ya uhakika ya Qur'an ni kukabiliana na adui mchokozi. Lazima tuwe na uchambuzi, ufafanuzi, utoaji wa maelezo sahihi, na simulizi za kweli kwa ulimwengu. Wengine wanasema kwamba tunapaswa kujadiliana, hilo ni kununua tu wakati (na kupoteza muda). Maadui walisambaratisha makubaliano ya JCPOA, kisha mwaka huu tulipokubali kufanya tena mazungumzo, wakafanya ulaghai kuingia nasi katika mazungumzo, lakini kwa kupitia mlango wa nyuma wakaunga mkono uvamizi wa ardhi yetu na kutangaza vita dhidi ya Iran. Historia yao ni ya ubaguzi wa rangi na uhalifu.

Alibainisha: "Lazima tueleze hali ilivyo uwanjani, na tukiwa katika hali ya vita, tufanye (tutekeleze) wajibu wetu na tuwepo uwanjani kikamilifu. Maelezo na ubainishaji sahihi na wa ukweli katika anga ya mtandao ni muhimu, na uwezo wa wajumbe na wamisionari (Mubalighina) wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (AS) lazima utumike vizuri."

Shahidi Soleimani alisema kuwa Iran ni Haram (Madhabahu), na ni lazima kuhifadhi nguzo za Haram (Madhabahu) hii. Leo, hatukabiliani na Israel pekee, bali tunakabiliana na nguvu zote zinazotaka kuharibu na kufuta katika ndimi zetu mazungumzo ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Nchi zote za Kiislamu lazima (ziwe Basiji - kwa maana) zihamasishwe. Hivi ni vita kamili na vya jumla (vya pande zote). Tumewekwa kwenye mtihani mkubwa, hivyo kila mtu, mahali popote alipo, lazima atimize wajibu wake. Leo hii hii ni vita vya imani dhidi ya ukafiri, kwa maana fulani, ni vita vya makundi (Ahzab) dhidi ya mfumo wa imani unaoongozwa na Imam Khamenei.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha