Iran imetangaza kuwa inajiandaa kwa mazungumzo muhimu ya kimataifa huku ikisisitiza utekelezaji wa makubaliano ya amani, kuzuia hujuma dhidi ya mchakato huo, na kupendekeza mpango mpya wa usimamizi wa Mlango wa Hormuz ndani ya siku 60.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baqaei, amesema kuwa mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya Iran kwa uungaji mkono wa Marekani yalishindwa kufikia malengo yake kutokana na uimara, mshikamano na kujitolea kwa wananchi wa Iran, hali iliyowageuzia washambuliaji hasara na kushindwa.
IRGC imesema imeharibu kituo cha anga kilichotumika katika shambulio dhidi ya mnara wa mawasiliano wa Kisiwa cha Sirik na kuonya kwamba mashambulizi yoyote yatakayojirudia yatakabiliwa na jibu kali zaidi.