Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul Bayt (as) - ABNA - Dokta Masoud Pezeshkian, katika kikao cha Baraza la Mawaziri Jumapili jioni hii, alitoa rambirambi kwa kuuawa shahidi kundi la makamanda wa ngazi za juu wa nchi pamoja na idadi kubwa ya watu wa nchi yetu, na kusisitiza haja ya kusimama dhidi ya hujuma za utawala wa Kizayuni, akisema: "Matukio haya kwa mara nyingine yalionyesha kuwa utawala wa Kizayuni hauzingatii kanuni zozote za kibinadamu, kisheria au za kimataifa."
Rais amekosoa kimya na uungaji mkono wa nchi za Magharibi hususan Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya kwa vitendo vya jinai vya utawala huo ghasibu unaoukalia kwa mabavu mji wa Jerusalem (Quds) na kusema: Badala ya kuzuia mashambulizi hayo ya kinyama, tunashuhudia silaha, kijasusi na uungaji mkono wa kisiasa kwa utawala huu. Ndege, makombora na silaha zilezile ambazo utawala huu unazo leo hii katika uchokozi wake dhidi ya nchi yetu zilitolewa na nchi hizo hizo za Marekani na Magharibi, na msaada wake wa kijasusi pia hutolewa kupitia mifumo yao ya rada na kijeshi.
Dakta Pezeshkian amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijawahi kutaka vita wala mizozo na kuongeza kuwa: "Hata hivyo, kama vile vikosi vyetu vya kijeshi likiwemo jeshi serikali na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lenye nguvu hadi sasa vimetoa majibu yanayofaa na yenye nguvu, iwapo hatua za kiuadui zitaendelea, majibu yatakuwa ya maamuzi na makali zaidi."
Rais ameutaja mchakato wa hivi sasa kuwa ni wa kishenzi na unaopingana na nara potofu za watetezi wa mazungumzo na ustaarabu na akasema: "Inatarajiwa kuwa nchi za Kiislamu na eneo zitachukua misimamo iliyo wazi, yenye maamuzi na madhubuti dhidi ya uchokozi wa utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake. Utawala unaofuata kila jinai katika eneo bila vikwazo vyovyote na kwa mwanga wa kijani wa Marekani."
Dakta Pezeshkian akimnukuu afisa mmoja wa Marekani amesisitiza kuwa: Kama ilivyoelezwa katika mazungumzo kati ya afisa wa Marekani na Dakta Araqchi, utawala wa Kizayuni hauwezi kuchukua hatua yoyote bila ya idhini ya Marekani, na tunayoyashuhudia leo yanafanywa kwa uungaji mkono wa moja kwa moja wa Washington; ingawa wanajaribu kuficha jukumu lao kwenye vyombo vya habari.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itatumia uwezo wake wote ili kuzuia madhara kwa wananchi: "Serikali kwa kushirikiana na taasisi zote zinazowajibika itafanya kazi kwa umoja na mshikamano ili kutoa huduma zenye tija kwa wananchi wapendwa wa nchi hii. Katika hali mbaya ya sasa, sote hatuna budi kuweka kando tofauti zetu na kusimama pamoja ili kudumisha mafungamano na umoja wa kitaifa."
Dakta Pezeshkian aliuona umoja na mshikamano kuwa ni ulazima usioepukika wa nchi hii leo hii, na, akizungumzia nafasi muhimu ya wananchi katika uwanja huu, alibainisha: Taifa la Iran daima limekuwa na litaendelea kuwepo kwenye eneo la tukio, na sisi, kwa kutegemea imani na uelewa wa kitaifa, tutatoa jibu linalofaa na la kuponda na kuangamiza kwa uchokozi wowote.
Insha Allah - Mwenyezi Mungu akipenda - , Na kwa neema Yake, Taifa adhimu la Iran litasimama dhidi ya utawala huu ghasibu na litaupondaponda utawala huu unaoikalia kwa mabavu Palestina na kufanya mauaji ya halaiki kwa sapoti ya wafuasi wake wanaowaunga mkono na wenye madai ya kuwa wastaarabu.
Your Comment