Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Akilaani mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya jengo la vyombo vya habari vya kitaifa, Rais wa Iran Dakta. Masoud Pezeshkian aliyataja kuwa ni dhihirisho la wazi la ushenzi wa wazi na ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa. Amesifu ushujaa na utulivu wa mwandishi huyo wa habari wa Iran katika nyakati muhimu na kuutaja uthabiti wake kuwa ni ishara ya muqawama wa taifa ambalo kamwe haliinami mbele ya vitisho na ghasia.
Jinai ya aibu ya utawala wa Kizayuni ya kushambulia mtandao wa habari wa Redio na Televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wakati wa matangazo ya moja kwa moja (Mubashara) ilifichua dhihirisho jingine la ukatili wa bayana na ushenzi usio na mipaka wa serikali hiyo haramu mbele ya macho ya walimwengu.
Mbali na kitendo hicho cha kinyama kilichokiuka sheria zote za kimataifa, jibu la kijasiri la mwandishi wa habari, Bi. Sahar Emami, liliongeza ukurasa mwingine wa dhahabu na mzuri katika kitabu cha historia ya mapambano na Muqawama wa Taifa kubwa la Iran.
Pezeshkiani, alipongeza hatua ya mwandishi huyo wa habari wakati wa matangazo ya moja kwa moja akisema: "Maitikio ya kupongezwa ya simba jike huyu wa Iran kwenye kipindi cha moja kwa moja cha televisheni ni ishara ya upinzani (Muqawamah), uthabiti na kutoweza kushindwa kwa taifa lenye ustaarabu wa muda mrefu dhidi ya kelele za utawala usiojulikana asili yake na usio na sura halali." Kwa kumalizia, alitoa shukurani zake kwa uungaji mkono na uelewa wa kila Mwananchi katika taifa kubwa la Iran, na akatoa shukrani zake kwa vikosi vya ulinzi vya nchi ya Iran katika nyuga za kijeshi na habari, ambavyo vimekuwa na jukumu la kujitolea kwa kila namna katika uwanja wa mapambano dhidi ya batili na ushetani wa kizayuni.
Your Comment