Sheikh Said Othman: "Imam Ali (a.s) anakumbukwa na Ulimwengu wote wa Kiislamu kuwa yeye ni Shujaa wa Kiislamu, aliyeupigania Uislamu, na kuuhami Uislamu kwa ushujaa wake na ujasiri wake, daima aliutetea uhai wa Uislamu na aliuheshimisha Uislamu kupitia Upanga wake, kama ambavyo Ummul - Muuminina Khadija (s.a) aliuhamia na kuuheshimisha Uislamu kupitia Mali yake".
Imam Ali (a.s) alipigwa upanga na mtu aliyejulikana kwa jina la Abdur Rahman bin Muljim Muradi (laana iwe juu yake milele). Imam Ali (a.s) alikufa Shahidi siku tatu baadaye katika usiku wa 21 wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Imam Ali bin Abi Talib (a.s) ni shakhsia wa pili mkubwa katika Uislamu baada ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), na anaelezwa katika historia ya Uislamu kuwa alikuwa jasiri na shujaa wa kupigiwa mfano, mwenye imani thabiti, mwenye akhlaki njema, mwenye elimu na uadilifu usio na kifani.