Umoja wa Kiislamu
-
Shahriari: Vitabu Vipya vya Jumuiya ya Kimataifa ya Taqrib ya Madhehebu za Kiislamu, vinaangazia Umoja na Ustaarabu Mpya wa Kiislamu
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Taqrib baina ya Madhehebu ya Kiislamu, Dkt. Hamid Shahriari, alieleza kuwa: “Kwa bahati nzuri, kwa kuweka vitabu katika mfumo wa kielektroniki kupitia tovuti ya maonyesho ya vitabu, mazingira mazuri yameandaliwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wadau na wageni wanaopendelea kufanya manunuzi yao kwa njia za kidijitali.”
-
Majlis ya Mazazi ya Imam Ridha (as) yafanyika Jamiat Al-Mustafa(s), Tanzania | Hadithi Toka Vyanzo vya Kisunni Zinathibitisha Makhalifa Kumi na Wawili
Lengo la Mazungumzo Haya ni: Kuleta maelewano baina ya Madhehebu za Kiislamu na kuonyesha kuwa msingi wa Uimamu na Ukhalifa wa Maimam Kumi na Wawili wa Ahlul-Bayt (a.s), wanaofuatwa na Waislamu wa Madhehebu ya Shia Ithna Ashari, una mizizi pia katika vyanzo vinavyokubalika vya Kisunni.
-
Mkutano na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt. Batlida Burian, pamoja na baadhi ya Masheikh wa Kishia na Kisunni.
"Tanga ni mfano wa kuigwa kwa utulivu wa kidini. Tuendelee kudumisha hali hii na kushirikiana kwa ajili ya maendeleo ya jamii yetu."
-
Kiongozi wa Mapinduzi: "Hakuna manufaa yoyote kwa Umma wa Kiislamu yaliyo juu ya Umoja"
Kiongozi Muadham wa Mapinduzi ameeleza katika Mkutano na wahusika wa Hajj na baadhi ya Waumini waliotembelea Nyumba Tukufu (Al-Kaaba) kwamba: "Muundo na sura ya nje ya ibada hii ni ya kisiasa kabisa, lakini maudhui ya vipengele vyake ni ya kiroho na ya ibada, ili manufaa ya Wanadamu wote yaweze kutimizwa. Na leo, faida kubwa kwa Umma wa Kiislamu ni 'Umoja na Ushirikiano' ili kutatua matatizo ya Ulimwengu wa Kiislamu. Ikiwa umoja huu ungelikuwepo, matatizo kama ya Gaza na Yemen yasingekuwepo."
-
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Umoja wa Madhehebu ya Kiislamu:
Udhalilishaji wa hivi karibuni wa mambo matukufu ya Waislamu wa Kisunni una nyanja tata zaidi
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kudumisha Umoja wa Madhehebu ya Kiislamu akilaani udhalilishaji wa mambo matukufu ya Waislamu wa Kisunni alisema: Udhalilishaji wa hivi karibuni una nyanja tata zaidi, na inatarajiwa kutoka kwa viongozi wa masuala haya kuchukua hatua za kuzuia kurudiwa kwa maafa kama haya.
-
Dr. Ali Taqavi, Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (s)Tanzania, akiambatana na Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum watembelea uwanja wa Michezo Zanzibar + Picha
Uislamu umesisitiza Umoja wa Kiislamu, na madhehebu yote ya Kiislamu yanaunganishwa na Umoja wa Kiislamu, na Kibla cha Waislamu wote ni kimoja, na Qur'an ndio Kitabu chao na Muongozo wao.
-
Je, jinai ya Palestina ni kweli kuwa inaungwa mkono na Iran ya Kishia?!
Wakati picha za kutisha za mauaji ya halaiki huko Gaza zimeamsha dhamiri za wanadamu kote ulimwenguni, ukimya mzito katika baadhi ya jamii za Kiislamu, haswa kati ya duru za kidini, unatia shaka. Kwa nini baadhi ya watu wanauita Upinzani (Muqawamah) huu "wa Kidini" au "Kisiasa" na kuondoa uungaji mkono wao wakati Hamas, Hezbollah, au Iran inaposimama dhidi ya Israel?!, Je, (kupinga) dhulma na ukandamizaji kwa Wapalestina unahitaji idhini ya Madhehebu?
-
Fat'wa Mpya: Kuitetea Palestina na Jihad dhidi ya Utawala wa Kizayuni ni Wajibu Ayn (jambo la faradhi kwa kila Mtu)
Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Ulimwenguni umetoa Fat'wa kuhusu Wajibu wa Jihadi katika kuunga mkono Ghaza na kusisitiza kuwa, Jihadi dhidi ya utawala wa Kizayuni na mamluki na askari wake wanaohusika na mauaji ya halaiki ya watu wa Ghaza katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina ni wajibu mutlaki (unaomgusa kila mtu).
-
Semina ya Mubaghilina wa Mkoa wa Kagera - Wilaya ya Muleba - Tanzania
Kauli mbio yetu ni: Kama Mubalighina ni kuhakikisha malengo ya Mtume (s.a.w.w) yanatimia kwa njia safi ya kuleta umoja, upendo na amani.
-
Wasifu wa Amirul Momineen (AS) unapaswa kuunganisha mwili wa Umma wa Kiislamu
Katika hotuba yake kwa mnasaba wa kuuawa shahidi Imam Ali, Waziri Mkuu wa Iraq alitaja fadhila za Imam Ali (a.s).