Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Tanga, Tanzania – Katika juhudi za kuimarisha mshikamano wa kijamii na kidini, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt.Batlida Burian alikutana leo na baadhi ya viongozi wa dini kutoka Madhehebu ya Kishia na Kisunni.
Mkutano huo ulifanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuhudhuriwa na Masheikh Mashuhuri wa Shia na Sunni.
Katika hotuba yake, Dkt.Batlida Burian alisisitiza umuhimu wa amani, mshikamano na maelewano baina ya Waumini wa dini zote, akisema:
"Tanga ni mfano wa kuigwa kwa utulivu wa kidini. Tuendelee kudumisha hali hii na kushirikiana kwa ajili ya maendeleo ya jamii yetu."
Masheikh walioshiriki walieleza kuridhika kwao na mkutano huo, wakikubaliana kuhusu haja ya kuimarisha mawasiliano ya mara kwa mara kati ya Madhehebu na kushirikiana katika shughuli za kijamii kama vile elimu, afya, na misaada kwa wahitaji.
Mkutano huo ulimalizika kwa maombi ya pamoja na ahadi ya kuendeleza ushirikiano wa karibu kwa ajili ya ustawi wa Tanga na taifa kwa ujumla.
Viongozi wa Kidini miongoni mwa waliohudhuria katika Mkutano huo ni pamoja na:
1_Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania, Sheikh Dkt.Alhad Mussa Salum.
2_Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-salaam - Tanzania, Hojjatul Islam wal-Muslimin, Dkt.Ali Taqavi.
3_Mkuu wa Taasisi ya Kiislamu ya Hojjatul Asr Foundation Tanzania, Sayyid Arif Naqvi.
Your Comment