5 Aprili 2025 - 23:07
Semina ya Mubaghilina wa Mkoa wa Kagera - Wilaya ya Muleba - Tanzania

Kauli mbio yetu ni: Kama Mubalighina ni kuhakikisha malengo ya Mtume (s.a.w.w) yanatimia kwa njia safi ya kuleta umoja, upendo na amani.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Pichani ni masheikh na maustadhi wa Madhehebu ya Ahlal-Bayt (as) wanaotoka katika sehemu tofauti kila mmoja wao, wengine wanaotoka maeneo ya vijiji, wengine maeneo ya kata, au mitaa na Wilaya.

Wamekutana kujadili Maendeleo ya Tabligh katika Maeneo mbalimbali Mkoani Kagera - Wilaya ya Muleba.

Semina ya Mubaghilina wa Mkoa wa Kagera - Wilaya ya Muleba - Tanzania

Walipata Picha ya Pamoja kwa ajili ya kumbukumbu baada ya kukutana pamoja na kujadili namna ya kuboresha na kupanua wigo wa harakati za Kishia kila mmoja katika maeneo yake.

Kikao hicho kimefanyika katika kijiji cha mishuro, kata Kasharunga, Wilaya ya Muleba, Mkoa wa Kagera.

Kauli mbio yetu ni: Kama Mubalighina ni kuhakikisha malengo ya Mtume (s.a.w.w) yanatimia kwa njia safi ya kuleta umoja, upendo na amani.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha