27 Mei 2025 - 01:13
Ayatollah Khamenei: Umoja wa Mataifa ya Kiislamu Ndiyo Njia Pekee ya Kudumisha Usalama wa Umma

Msimamo wa Pakistan kuhusu suala la Palestina umekuwa wa kupongezwa sana. Wakati daima kumekuwa na vishawishi kwa nchi za Kiislamu kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni, Pakistan haijawahi kushawishika na vishawishi hivyo.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Sayyid Ali Khamenei katika kikao na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif amesema:

1_Tunafurahia kusitishwa kwa migogoro kati ya Pakistan na India, na tunatumaini kuwa migogoro kati ya nchi hizi mbili itatatuliwa.

2_Msimamo wa Pakistan kuhusu suala la Palestina umekuwa wa kupongezwa sana. Wakati daima kumekuwa na vishawishi kwa nchi za Kiislamu kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni, Pakistan haijawahi kushawishika na vishawishi hivyo.

3_Wakati ambapo wachochezi wa vita duniani wana nia nyingi za kuanzisha migogoro na vita, njia pekee ya kuhakikisha usalama wa Umma wa Kiislamu ni umoja wa mataifa ya Kiislamu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha