migogoro
-
Rais Pezeshkian Atoa Wito wa Kudhibiti Matumizi ya Nishati Ili Kuepusha Migogoro
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, amesisitiza umuhimu wa kupunguza na kusimamia matumizi ya nishati kama njia kuu ya kuzuia migogoro ya nishati, huku akipendekeza matumizi ya nishati ya jua katika shule.
-
Jenerali Abdullahi: Nchi zitakazomtegemea Marekani kama ngao ya ulinzi zitaingia kwenye moto wa vita
Kamanda wa Makao Makuu ya Kati ya Khatam al-Anbiya (s.a.w), Jenerali Ali Abdullahi, ameonya nchi za eneo hilo dhidi ya kutegemea Marekani kwa ulinzi, akisema utegemezi huo unaweza kuzifanya kuwa sehemu ya migogoro na vita.
-
Waziri Mkuu wa Iraq Aagiza Kuimarishwa kwa Tahadhari na Ulinzi wa Kijeshi Nchini Kote
Msemaji wa Amiri Jeshi Mkuu wa Iraq amesema Waziri Mkuu ameagiza kuongezwa kwa kiwango cha tahadhari na utayari katika kambi na vituo vyote vya kijeshi, pamoja na kuharakisha uimarishaji wa mifumo ya rada, ulinzi wa anga na mipango ya kiintelijensia ili kuzuia vitisho vyovyote vya kiusalama.
-
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran: Tukilazimishiwa Vita, Tutajilinda kwa Nguvu na Uwezo
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Reza Aref, amesema Iran haitafuti vita wala migogoro, bali inaamini katika mazungumzo, lakini endapo italazimishiwa vita itajilinda kwa nguvu na uwezo mkubwa.
-
Rais wa Iran Aishukuru Qatar kwa Jukumu Lake la Kupunguza Mvutano na Kuendeleza Diplomasia
Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, ameipongeza Qatar kwa mchango wake katika kupunguza mvutano wa kikanda na kuwezesha juhudi za kidiplomasia zilizopelekea kufikiwa kwa makubaliano ya kumaliza vita.
-
Baghaei: Nguvu Waliyoiumba kwa Ajili ya Kuwatawala Wengine Imetoka Mikononi Mwao
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa wale wanaotumia machafuko kama njia ya kutawala mataifa mengine huishia kuwa watumwa wa machafuko hayo. Ameonya kwamba nguvu iliyoundwa kwa ajili ya kuwatawala wengine hatimaye huweza kutoka katika udhibiti wa walioiunda.
-
Ayatollah Mojtaba Khamenei Aonya Dhidi ya Njama za Kusababisha Mgawanyiko wa Kijamii Iran
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza umuhimu wa kulinda umoja wa wananchi, akionya kuwa adui anatumia mbinu za kueneza mifarakano ya kijamii baada ya kushindwa kufikia malengo yake kupitia mashinikizo ya kijeshi, kiuchumi na kisiasa.
-
Iraq yakataa kuruhusu matumizi ya anga lake kwa mashambulizi dhidi ya Iran
Tamko la Iraq linaonyesha kuwa Iraq inalinda mamlaka yake na haitaki kuhusishwa na migogoro ya kijeshi katika eneo hilo, ikisisitiza sera ya kudumisha usalama na utulivu wa kikanda.
-
Mwenyekiti wa JMAT–TAIFA: Tukipendana na Kusaidiana Tutajenga Amani ya Taifa Letu
Akizungumza kuhusu msingi wa amani, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania alibainisha kuwa amani ya kweli huanzia katika mahusiano mema yanayojengwa kwa kujali, kuthaminiana na kusaidiana. Alieleza kuwa kitendo cha kusaidiana huondoa chuki na uhasama, kwani mtu anaposaidiwa huhisi kukubalika na kuheshimiwa, hali inayojenga imani na kuimarisha mshikamano wa kijamii.
-
Kwa mwaka wa tatu mfululizo; Sudan yaongoza orodha ya migogoro ya kibinadamu duniani
Sudan kwa mwaka wa tatu mfululizo imeorodheshwa juu kabisa katika orodha ya migogoro ya kibinadamu duniani.Nchi nyingine zilizoorodheshwa katika ripoti hiyo ni pamoja na: Myanmar, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mali, Burkina Faso, Lebanon, Afghanistan, Cameroon, Chad, Colombia, Niger, Nigeria, Somalia, Syria, Ukraine na Yemen.
-
Watafiti: Sera za Jolani zimeiingiza Syria katika lindi la machafuko
Wataalamu wameonya kwamba kuendelea kwa vurugu na sera za kueneza mgawanyiko kunaisukuma Syria kuelekea migogoro iliyo kubwa na ya kina zaidi.
-
Iran Yajitolea kusimama Kati Katika Mvutano Kati ya Pakistan na Afghanistan
Wataalamu wa masuala ya kikanda wanasema kwamba mpatanishi wa tatu (Iran) anaweza kusaidia kupunguza hatari za mzozo mkubwa na kuimarisha ushirikiano na amani katika eneo hilo.