27 Juni 2025 - 13:38
Uongo wa Trump kuhusu kushambulia vinu vya Nyuklia vya Iran ni Mbinu za Propaganda. Zijue mbinu hizo na jinsi zinavyotumika, hasa katika siasa

Kutumia hofu au hisia kali Kujenga hofu, hasira, au mshangao kwa ujumbe fulani kunasaidia kuimarisha ujumbe na kuufanya uonekane wa dharura au muhimu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mbinu za Propaganda anazozitumia Trump kuhusu kulazimisha Dunia iamini Uongo wake kuwa ameshambulia na kufuta kabisa vituo vya Nyuklia vya Iran, kawaida mbinu hizo hujulikana kama mbinu ya:

1-Kurudia kauli au ujumbe mara kwa mara

Hii ni Mbinu ya kisiasa kama Trump anavyoitumia kwenye siasa zake na kuitisha CNN Kwa hatua yake ya kukadhibisha Uongo wake hadharani – Ni Mbinu ya kurudia madai ya vituo vya nyuklia vya Iran kuharibiwa na kutaka Dunia imuamini hata kama hakuna ushahidi. 

"Kurudia" uongo mara kwa mara, huweza kufanya watu waanze kuamini, hata kama si kweli kabisa. 

Mbinu hii inaitwa “illusory truth effect” (athari ya ukweli wa kudanganya).

2-Kupotosha au kupunguza ukweli

Propaganda haina lazima iwe uongo kabisa, inaweza kuwa mchanganyiko wa ukweli na uongo, au kuondoa vipengele muhimu ili kubadilisha mtazamo wa hadhira.

3-Kutumia hofu au hisia kali
Kujenga hofu, hasira, au mshangao kwa ujumbe fulani kunasaidia kuimarisha ujumbe na kuufanya uonekane wa dharura au muhimu.

4-Kushambulia Wapinzani

Kwa kuwawekea alama za utovu wa nidhamu, uwongo, au udhaifu kwa wapinzani ili kuwatenga na kuwafanya watu wasiwe na imani nao.

5-Kuunda hadithi rahisi na zinazogusa hisia

Hadithi au ujumbe rahisi kueleweka, wenye taswira za wazi, huwa rahisi kuenziwa na kukumbukwa.

Mbinu Hizi Katika Siasa

Katika siasa, viongozi hutumia propaganda ili kuimarisha ushawishi wao na kudhibiti mtazamo wa watu, hasa wakati wa mgogoro au kampeni. 

Hii inaweza kuwa njia ya kupunguza wasiwasi wa umma, kuunda hadhi ya Kiongozi mwenye nguvu, au kuipa nchi picha ya usalama na uthubutu.

Kwa Nini Hii Inakuwa Hatari?

Inapotosha maamuzi ya umma: Watu wanapokuwa na habari zisizo sahihi, huweza kufanya maamuzi mabaya kuhusu masuala ya kitaifa na kimataifa.

Inaleta mgawanyiko: 

Propaganda hii ya uongo inaweza kueneza chuki na mgawanyiko kati ya jamii au mataifa.

Inahatarisha amani

Katika muktadha wa masuala kama nyuklia au vita, propaganda inaweza kuongeza mivutano na hatimaye kusababisha migogoro ya kijeshi.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha