Donald Trump
-
Rais wa Iran: Mazungumzo na Marekani “Hayana Maana”
Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema kuwa mazungumzo na Marekani hayana maana kwa sasa, akieleza kuwa Tehran imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi baada ya kushiriki katika mazungumzo, pamoja na vikwazo, shinikizo na vitisho.
-
Washington Post: Trump Akishindwa, Atakuwa “Rais wa Kipindi cha Mpito”
Gazeti la Washington Post katika uchambuzi wake limeandika kuwa iwapo Democrats watapata udhibiti wa Seneti na Baraza la Wawakilishi la Marekani katika uchaguzi wa katikati ya muhula, Donald Trump kwa vitendo atageuka kuwa “Rais wa kipindi cha mpito”, huku akikabiliwa na vikwazo zaidi katika kuendelea na kipindi chake cha urais.
-
Trump Arudia Tena Dai la Kushindwa kwa Iran
Donald Trump, Rais wa Marekani, katika hotuba yake leo (Jumanne), alidai kwamba Iran imeshindwa vibaya sana na iko katika hali mbaya mno, akisema kuwa mzozo huu utamalizika hivi karibuni.
-
Gazeti la Kiebrania: Netanyahu na Trump Wanaacha Athari Kubwa ya Uharibifu Nyuma Yao
Gazeti la Maariv limechapisha makala inayokosoa mwenendo wa uongozi wa Benjamin Netanyahu na Donald Trump. Gazeti hilo linasema Israel na Marekani zinakabiliwa na migogoro ya utambulisho na kudhoofika kwa baadhi ya taasisi. Kwa mujibu wa makala hiyo, Netanyahu na Trump wanatajwa kuwa na ajenda za kibinafsi, kikabila na kijamii ambazo gazeti hilo linazitathmini kuwa hazina misingi ya kidemokrasia.
-
Afisa wa IRGC: Trump Ananufaika Kifedha Kutokana na Vita na Iran
Mshauri mwandamizi wa Kamanda Mkuu wa IRGC amesema maamuzi ya Donald Trump katika mzozo unaoendelea na Iran yanaendeshwa na maslahi binafsi. Amesema baadhi ya maamuzi hayo yanahusishwa pia na maslahi ya kampuni na taasisi zinazohusishwa na rais huyo wa Marekani. Kauli hiyo imetolewa katika muktadha wa mvutano unaoendelea kati ya Marekani na Iran.
-
Washington Post: Marekani imewaacha Wasaúdi bila msaada wakati wa shinikizo la vita
The Washington Post imeripoti kuwa licha ya ushirikiano wa kiusalama wa miongo kadhaa kati ya Marekani na Saudi Arabia, Washington haijaingilia moja kwa moja kijeshi katika mgogoro wa sasa. Hali hiyo imeiacha Riyadh ikikabili vitisho dhidi ya miundombinu yake ya mafuta na kijeshi huku ikibeba sehemu kubwa ya mzigo wa kukabiliana na vitisho hivyo.
-
Foreign Policy: Marekani inashindwa katika vita dhidi ya Iran kwa karibu kila upande
Jarida la Foreign Policy limeeleza kuwa vita dhidi ya Iran vimekuwa “janga la kimkakati” kwa Washington, likisema Marekani imeshindwa kufikia malengo yake makuu ya kimkakati. Jarida hilo pia limekosoa madai ya Donald Trump kuhusu “ushindi” na kueleza kuwa mapigano yanaendelea huku kukiwa hakuna dalili wazi ya makubaliano kati ya Washington na Tehran.
-
Seneta Mshirika wa Trump: Uwezekano wa Marekani Kutuma Vikosi vya Ardhini Iran ni Sifuri
Seneta Ted Cruz amesema uwezekano wa Marekani kutuma mamia ya maelfu ya wanajeshi wa ardhini nchini Iran na kurudia kisa cha uvamizi wa Iraq ni “sifuri”, akisisitiza kuwa Rais Donald Trump hataki kuchukua mkondo huo.
-
Trump Ajaribu Kuigeuza Hormuz kuwa “Eneo la Marekani” kwa AI, Wakati Iran Yatekeleza Operesheni Halisi
Rais wa Marekani Donald Trump amewahi kuzungumzia kuifanya Mlango-Bahari wa Hormuz kuwa eneo la Marekani, huku Iran ikitekeleza operesheni za kijeshi katika njia hiyo muhimu na kutangaza kukamata ndege-drone ya chini ya maji ya Marekani.
-
CNBC: Thamani ya Uwekezaji wa Trump katika Sekta ya Mafuta Yaongezeka Wakati wa Vita vya Iran
Uchambuzi wa CNBC umebaini kuwa thamani ya hisa na uwekezaji wa Rais wa Marekani, Donald Trump, katika kampuni za mafuta na gesi iliongezeka katika miezi sita ya mwanzo ya vita vya Iran.
-
Rais Pezeshkian Amjibu Trump: Iran Itaendelea na Upinzani Hadi Wavamizi Wajute Sana
Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kupinga kwa nguvu zote hadi wavamizi wajute sana, huku ikiendelea kutetea haki za wananchi wa Iran.
-
Waziri wa Zamani wa Ulinzi wa Marekani: Trump Amejinasua Njia katika Vita dhidi ya Iran
Leon Panetta amesema Marekani na Iran zimekwama katika mkwamo mkubwa wa kivita, huku akionya kuwa vita hivyo vinaweza kuendelea kwa miezi mingine sita na kugeuka kuwa vita visivyo na mwisho Mashariki ya Kati.
-
Mafuta ya Venezuela Hayatakuwa Suluhisho la Haraka la Kujaza Akiba ya Kimkakati ya Mafuta ya Marekani
Licha ya Marekani kutangaza mpango wa kutumia mafuta ya Venezuela kujenga upya akiba yake ya kimkakati ya mafuta (SPR), kiwango cha sasa cha uzalishaji wa Venezuela na changamoto za miundombinu vinaifanya kuwa suluhisho la muda mrefu badala ya kuweza kuziba haraka pengo kubwa la akiba ya mafuta ya Marekani.
-
Waandishi Watatu Wafunguliwa Kesi Dhidi ya Hegseth na Pentagon kwa Madai ya Udhibiti wa Vyombo vya Habari
Waandishi watatu wa gazeti la kijeshi la Stars and Stripes wamefungua kesi katika mahakama ya shirikisho dhidi ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth na maafisa wengine wa Pentagon, wakidai kuwa walifukuzwa kazi kwa kulinda uhuru wa vyombo vya habari na kuripoti kuhusu hali mbaya ya wafanyakazi wa manowari ya ndege ya USS Abraham Lincoln.
-
Mohsen Rezaei: Madai ya njama ya Iran kumuua mtoto wa Trump ni propaganda za uongo za Netanyahu
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Meja Jenerali Mohsen Rezaei, amekanusha madai ya kuwepo kwa njama ya Iran ya kumuua mtoto wa Trump, akiyataja kuwa ni propaganda zilizobuniwa na hila za Benjamin Netanyahu.
-
Mtafiti wa zamani wa Pentagon: Marekani imekumbwa na kushindwa kimkakati dhidi ya Iran
Afisa wa zamani wa Pentagon, Jason Campbell, amesema serikali ya Trump bado haiko tayari kukubali rasmi kwamba mzozo huo umekuwa kushindwa kimkakati kwa Marekani.
-
Gharibabadi: Dhana potofu ya Trump kuhusu Mlango wa Hormuz itasahihishwa hivi karibuni
Iran: Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya Kisheria na Kimataifa, Kazem Gharibabadi, amejibu hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kuchapisha ramani inayoonyesha Mlango wa Hormuz kama “ardhi mpya ya Marekani”, akisema kuwa “dhana potofu ya Trump kuhusu Mlango wa Hormuz itasahihishwa hivi karibuni.”
-
The Atlantic: Trump awalipisha Korea Kusini gharama ya kushindwa kwake dhidi ya Iran
Jarida la The Atlantic limeandika kuwa Donald Trump, badala ya kukubali jukumu la kushindwa katika vita dhidi ya Iran, ameelekeza shinikizo kwa washirika wa Marekani. Jarida hilo linasema Korea Kusini imekuwa miongoni mwa walengwa wa hatua hizo, licha ya kuwepo kwa makumi ya vichwa vya nyuklia vya Korea Kaskazini.
-
Qalibaf: Trump Alisaini Kutambua Kambi ya Upinzani (Muqawama)
Qalibaf amesema Donald Trump, wakati wa kusaini Mkataba wa Maelewano, alisaini pia utambuzi wa Kambi ya Upinzani kwa lugha ya Kiajemi, baada ya Marekani kutaka Iran iachane na makombora, harakati za Upinzani, mpango wa nyuklia na suala la Mlango wa Hormuz.
-
Vyombo vya Habari vya Iran Vyaripoti Mahali Alikojificha Donald Trump Wakati wa “Operesheni Taco”
Ripoti hizo za vyombo vya habari vya Iran zinadai kuwa operesheni hiyo ilihusisha mbinu za siri za uhamisho wa anga, ambapo Trump alitolewa Air Force One na kupelekwa kwenye ndege ya kijeshi akiwa amejificha ndani ya sehemu ya mizigo ya chakula na vinywaji.
-
Trump: Tulikabili Hatari Kubwa, Ikiwemo Uwezekano wa Kuuawa, Wakati wa Kuondoka Uturuki
Donald Trump alidai kuwa Marekani “inadhibiti kikamilifu” Mlango wa Hormuz, akisema: “Siitambui Iran kama nchi ya kuaminika, na tunadhibiti kikamilifu Mlango wa Hormuz.”
-
Qalibaf kwa Marekani: Kubalini Ukweli na Timizeni Ahadi Zenu
Spika wa Bunge la Iran amesema kauli za Rais wa Marekani ni sehemu ya diplomasia ya maonyesho isiyo na tija, akisisitiza kuwa vitisho, ahadi zisizotekelezwa na taarifa za upotoshaji haziwezi kuleta mafanikio katika mazungumzo.
-
Mamilioni Waadhimisha Arubaini Karbala; Sheikh Naim Qassem Asisitiza Muqawama Itaendelea Hadi Uvamizi Utakapokoma
Mamilioni ya waumini wamekusanyika Karbala na maelfu wengine Baalbek nchini Lebanon kuadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (as). Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Hezbollah, Sheikh Naim Qassem, amesema muqawama utaendelea hadi Israel itakapojiondoa kikamilifu katika maeneo inayoyakalia.
-
Mtaalamu wa Marekani: Trump Anajua Mwenyewe Kuwa Iran Haitasalimu Amri
Mchambuzi wa siasa kutoka Chuo Kikuu cha Chicago, Robert Goloty, amesema kuwa hata Donald Trump anatambua kuwa Iran haiwezi kulazimishwa kusalimu amri, na kauli zake kuhusu kujisalimisha kwa Tehran zinaweza kuwa sehemu ya mkakati wa kisiasa wa kupata uungwaji mkono kutoka kwa makundi ya mrengo mkali wa kulia.
-
New York Times: Trump Anakabiliwa na Changamoto ya Kuelewa Viongozi wa Iran
Gazeti la New York Times limesema kuwa Donald Trump ni miongoni mwa marais wa Marekani waliokumbana na ugumu mkubwa wa kuelewa mfumo wa uongozi wa Iran, hali iliyochangia kuongezeka kwa msuguano kati ya Washington na Tehran.
-
Ansarullah: Mabadiliko ya Kauli za Trump Yamesababishwa na Nguvu ya Uzuiaji ya Iran
Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kubadilika kwa kauli za Donald Trump kuelekea lugha ya amani kunatokana na kutambua hali halisi ya uwanja na uwezo wa Iran wa kuzuia vitisho vya kijeshi katika eneo hilo.
-
Seneta wa Marekani Amkosoa Trump kwa Kumteua Jared Kushner Kushughulikia Mazungumzo na Iran
Seneta wa Chama cha Democratic nchini Marekani, Mark Kelly, amesema Jared Kushner hastahili kuongoza mazungumzo na Iran, akimtaka Rais Donald Trump kumteua mtu mwenye uwezo na uzoefu badala ya kumkabidhi jukumu hilo mkwe wake.
-
Mwandishi wa Marekani: Trump Hana Ujasiri wa Kuanzisha Vita Dhidi ya Iran
Mwandishi na mwanahabari wa Marekani Ethan Levins amesema kuwa Rais Donald Trump hana uwezo wa kuanzisha vita dhidi ya Iran, akidai kuwa matamshi yake ya vitisho yana lengo la kuiridhisha Israel kuliko kuonyesha nia ya kuchukua hatua za kijeshi.
-
NBC: Trump Aripotiwa Kukerwa na Tofauti za Maoni Miongoni mwa Maafisa wa Marekani Kuhusu Iran
Ripoti ya mtandao wa NBC inaeleza kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump, alionesha kutoridhishwa na tofauti za maoni zilizojitokeza miongoni mwa maafisa wake wa usalama wa taifa kuhusu mkakati wa kuendelea na operesheni dhidi ya Iran.
-
Mashambulizi ya Saudi Arabia na Marekani dhidi ya Hashd al-Shaabi Yazua Maswali Kufuatia Ziara ya Waziri Mkuu wa Iraq Marekani
Mashambulizi yaliyotekelezwa na Saudi Arabia na Marekani dhidi ya vituo vya Hashd al-Shaabi yamesababisha vifo vya zaidi ya wanajeshi 20 wa Iraq, huku yakizua mjadala kuhusu matokeo ya ziara ya Waziri Mkuu mpya wa Iraq nchini Marekani na mkutano wake na Rais wa Marekani, Donald Trump.